Home Kimataifa 17/8/2018 Cr7 huyu hapa Stadio MarcAntonio kwa mara ya kwanza katika Serie...

17/8/2018 Cr7 huyu hapa Stadio MarcAntonio kwa mara ya kwanza katika Serie A, DSTV nao hawachezi mbali

10138
0

Tarehe 29 August mwaka 2009 Cristiano Ronaldo alivaa jezi ya Real Madrid kwa mara ya kwanza katika mechi ya la Liga, miaka 9 baadaye anavaa jezi ya Juventus mwezi August lakini tarehe 17 akiichezea Juventus mchezo wa kwanza Serie A vs Chievo.

Mchezo kati ya Chievo vs Juventus unakwenda kupigwa saa moja usiku katika dimba la nyumbani la Chievo (Stadio MarcAntonio), na DSTV watarusha moja kwa moja mchezo huu kutoka Italia na sasa unaweza kuuangalia kupitia Lap Top yako, Simu au Tablet kama ukiwa na application ya DSTV.

Msimu uliopita tulishuhudia Juventus wakitwaa taji la 7 mfululizo la Serie A, Bianconeri sasa wanataka kuweka rekodi ya kushinda taji la 8 la Scudetto.

Juve wamefanya usajili wa kujiimarisha katika – usajili mkubwa ukiwa ulioshitua watu wengi, usajili wa Cristiano Ronaldo na leo atacheza mchezo wake wa kwanza.

Usajili wa mwingine wa Bianconeri msimu huu umehusisha golikipa Mattia Perin kutoka Genoa akija kumsaidia Wojciech Szczesny, Emre Can nae alijiunga na Juve akitokea Liverpool. Wakati beki wa kulia wa Ureno, Joao Cancelo alisajiliwa kutoka Valencia na Leonardo Bonucci akarejea kutoka Milan.

Baada ya kumaliza katika nafasi ya 13, pointi 5 juu ya ukanda wa walioshuka daraja – msimu huu, Flying Donkeys wanataka kujiimarisha kwenye msimamo. Mchezaji wao wa zamani, Lorenzo D’Anna alichukua majukumu ya ukocha katikati ya msimu uliopita na kuwasaidia kuepuka kushuka daraja na sasa amepewa nafasi nyingine ya kuwaongoza.

Usajili wao umehusisha kiungo wa Nigeria Joel Obi kutoka Torino, mshambuliaji mzoefu wa Serie A, Filip Djordjevic kutoka Lazio, beki Luca Rossettini kutoka Genoa na hii leo wana advantage kwa kuanza katika dimba lao la Stadio Marcantonio Bentegodi.

Kibibi kizee cha Turin kilipata ushindi mara mbili msimu uliopita dhidi ya Chievo, wakishinda nyumbani wa Allianz Stadium mnamo September 2017, na Stadio Bentegodi mnamo January 2018.

Mara ya mwisho Juventus walipokutana na Chievo katika mchezo wa ufunguzi wa ligi – ilikuwa msimu 2014/15 katika dimba la Bentegodi – Juventus walishinda 0-1 kwa goli la kujifunga na Cristiano Biraghi – huu ndio ulikuwa mchezo wa kwanza wa Massimiliano Allegri akiwa mwalimu wa Juventus.

Katika michezo 12 kati ya Chievo na Juventus ,Chievo wamefunga mara mbili tu na huku katika alama 36 katika mechi zao walizocheza Chievo alipata alama moja tu huku Juventus wakipata 35.

Vikosi vinavyoweza kuanza.

Chievo. Wamemnunua Joel Obi, Mariusz Stepinskona Emmanuele Giaccherini na kocha Lorenza D’Anna anaweza kuwaingiza katika mfumo wake wa 4-3-3.

Juventus. Baada ya Buffon kuondoka Juventus alikokaa kwa muda ni wazi sasa Mattia Perin atakaa katika lango la Juve msimu huu.

Ujio wa Leornado Bonucci unaifanya pacha yake na Chiellini kurejea upya na upande wa mashambulizi Paulo Dyabala, Cristiano Ronaldo na Douglas Costa ndio wanaweza kuongoza mashambulizi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here