Home Kitaifa TFF yaruhusu vilabu kusajili wachezaji saba wa kigeni

TFF yaruhusu vilabu kusajili wachezaji saba wa kigeni

487
0
SHARE

tffHatimaye Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limebariki kuongezwa kwa wachezaji wa kigeni kwa vilabu vya ligi kuu Tanzania bara kwa msimu ujao, ambapo sasa kila klabu itaruhusiwa kusajili wachezaji saba ikiwa ni ongezeko la wachezaji wawili kutoka kwenye idadi ya awali ya wachezaji watano .

Maamuzi hayo yamefanywa leo na kamati ya utendaji ya TFF ambayo ilikaa mjini Zanzibar na kupitisha mapendekezo hayo yaliyoombwa na vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo.

Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa amesema, kikao hicho kimeridhia kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni watakao ruhusiwa kusajiliwa na vilabu vya ligi kuu lakini kutakuwa na utaratibu maalumu wa kufuata kabla ya wachezaji hao hawajapewa ruhusa ya kukipiga kwenye ligi kuu Tanzania bara.

“Kwanza nitamke wazi kwamba leo kamati ya utendaji ya TFF iliketi katika ukumbi wa maktaba wa wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na michezo hapa Zanzibar, kamati ya utendaji imeamua kwamba katika msimu mpya wa ligi wachezaji wa kigeni watakao ruhusiwa kusajiliwa ni saba na wote watauhusiwa kuanza”, amesema Mwesigwa.

“Lakini vilevile ilikwenda mbali zaidi na kuamua kwamba sasa wachezaji wa kigeni wanaokuja kucheza hapa Tanzania wanatakiwa wawe ama wanacheza kwenye timu zao ‘senior’ timu kwa maana ya timu ya taifa ya wakubwa, U23, U20 au U17 vinginevyo kama hawana sifa hizo basi wawe wanacheza kwenye klabu ya ligi kuu ambayo inatambuliwa”, ameeleza.

“Ukaguzi utakuwa unafanyika wakati mchezaji anaposajiliwa, maombi yataletwa watalipa ‘fee’ tutakagua kama hiyo fee imelipwa, na tunaita hiyo fee kwamba ni ‘development fee’ ambayo watatakiwa kuilipa dola 2,000 kwa msimu kwa kila mchezaji wa kigeni pesa ambazo zitaenda kuimarisha maendeleo ya soka. Pia kuna mambo mengi yanaangaliwa kwa mchezaji mwenyewe, tutaangalia kama leseni yake imetoka au kama amepata ‘permit’”, amefafanua.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here