Home Kimataifa Thamani ya Juve yaongezeka kwa €160m zaidi ndani ya siku 3 –...

Thamani ya Juve yaongezeka kwa €160m zaidi ndani ya siku 3 – CR7 kuwa balozi wa Ferrari duniani

20386
0
SHARE

Juventus wameanza kuonja mafanikio ya kuhusishwa na Cristiano Ronaldo tayari, thamani ya klabu imepanda kwa asilimia 22 ndani ya siku 3 – thamani ya klabu imeongezeka kwa zaidi ya €160m.

Wakati uhamisho wa €100m kwenda Turin ukizidi kuripotiwa tokea Jumatatu wiki – huku wengine wakiripoti kwamba huenda dili hilo litakamilika kufikia jumamosi hii – bado kumekuwepo na maswali Bianconeri wataweza vipi kuhimili gharama za CR7.

Ripoti kutoka kwenye soko la hisa – thamani ya klabu ya Juventus imekuwa kwa asilimia 22 – mtajinwa klabu umekuwa kutoka €665m mpaka €825m, kwa mujibu wa Calcio e Finanza.

Kwa upande wa Ronaldo atakuwa analipwa mshahara pekee €30m sawa na zaidi ya billioni 80 kwa mwaka – kabla ya kupata maslahi mengine. Makampuni mengine ya familia ya mmiliki wa Juventus bwana Agnelli (Ferrari, FIAT and Jeep) – yatasaidia kwenye ulipaji wa mshahara huo.

Cristiano pia anatarajiwa kupewa mkataba mwingine wa kumongezea kipato kwa kufanywa kuwa balozi wa Ferrari duniani. Mkataba ambao utamuingizia kiasi kingine cha €20m

Kwa maana hiyo tayari Ronaldo kupitia mahusiano yake na Juventus moja kwa moja yatamuingizia kiasi cha €50m kwa mwaka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here