Home Kitaifa Mbao FC inaongoza ligi nini kipo nyuma ya pazia?

Mbao FC inaongoza ligi nini kipo nyuma ya pazia?

8424
0

Klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza kwa ndio inaongoza ligi kwa sasa ikiwa na pointi saba (7) baada ya kucheza mechi tatu na kufanikiwa kushinda michezo miwili na kutoka suluhu mchezo mmoja.

Matokeo ya Mbao FC katika mechi tatu za kwanza za msimu huu kwenye ligi: Alliance 0-1 Mbao, Stand United 1-2 Mbao, Singida United 0-0 Mbao.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Solly Njashi ameeleza kinachoifanya Mbao kufanikiwa katika mechi za kwanza za msimu huu.

“Ushirikiano wa wachezaji, viongozi na mashabiki pamoja na wadhamini nadhani ni vitu ambavyo vikiungana pamoja vinaleta ushindi hivyo naamini kama tutaendelea kushirikiana na umoja huu uliopo tutaweza kufanya vizuri.”

“Msimu huu tumebaki na wachezaji wengi, wapo walioondoka lakini waliobaki ni wengi. Nimejifunza kitu, wachezaji wengi wanapobaki baada ya dirisha la usajili wakiungana na wachache waliosajiliwa kuna kitu kinaongezeka.”

“Lakini kila mwalimu ana-falsafa yake hatuwezi kuzungumzia sana hilo lakini ndio safari imeanza tutaona huko mbele itakuaje.”

Udhamini

Sisi tuna mdhamini (GF Trucks & Equipment) ambaye tunaendelea nae tunapokwama tunasaidiana uongozi na mdhamini. Katika timu kuna mambo mengi wachezaji wakikubali kucheza, mashabiki, viongozi na wadhamini wakitekeleza wajibu wao hakuna sehemu ya mnaweza kukwama lakini kiukweli ugumu wa uandeshaji timu upo.”

“Msimu uliopita pia tulianza vizuri kwa kushinda mchezo wa kwanza lakini tukapoteza mechi mbili zilizofuata lakini msimu huu tumeweza kupata pointi 7 katika mechi tatu za kwanza.”

“Kuongoza ligi ni jambo jingine lakini pia kuendelea kubaki katika nafasi hiyo ni jambo la pili. Wadau wote wa Mwanza inabidi tuungane kuhakikisha tunabaki hapa, kila timu inapenda kuongoza ligi lakini ili kuongoza ligi inabidi kila mtu atimize wajibu wake.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here