Home Kitaifa “Ajib ana dhahabu miguuni mwake ila hajui”-Zahera Mwinyi

“Ajib ana dhahabu miguuni mwake ila hajui”-Zahera Mwinyi

13557
0

Na Tima Sikilo

KOCHA Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ‘Papaa’, amesema Ibrahim Ajibu ni mchezaji mwenye dhahabu miguuni mwake lakini bado hajalijua hilo.

Papaa amesema ameamua kumfungia kazi Ajibu katika mazoezi na anaamini baada ya muda mfupi atakuwa mpya.

Amesema kikosi chake kinawachezji wengi wazuri lakini Ajibu ni mchezaji mwenye akili ya mpira zaidi lakini kunavitu vichache ambavyo vinamgharimu hususan katika mazoezi

“Wachezaji wote ni wazuri lakini Ajibu anakitu cha ziada, ni mchezaji mwenye akili ya mpira lakini hajijui, anakaa na dhahabu miguuni mwake lakini hajui-Zahera Mwinyi.

Amesema atahakikisha anamkazia mchezaji huyo katika mazoezi ili aweze kuwa mpya na kutambua uwezo alionao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here