Home Kitaifa Alichosema Mwl. Kashasha kuhusu goli la Fei Toto

Alichosema Mwl. Kashasha kuhusu goli la Fei Toto

7432
0

Asikwambie mtu, Fei Toto alifunga bonge la bao kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara Yanga vs Ruvu Shooting goli ambalo limewasisimua wengi.

Sasa magoli kama haya Mwl. Kashasha huwa anayapa majina yake, bahati nzuri wakati naangalia mechi hiyo nilikuwa pia namsikiliza kupitia radio akiwa pamoja na Enock Bwigane.

“Dakika ya 78 Feisal Salum ‘Fei Toto’, Fei Totoo…amepiga mpira mmoja kama ‘Zezou’ vile kule ni kwenye tundu ambako anatagia njiwa na kuiandikia Yanga bao la pili na anashangilia huku amevua jezi”-Bwigane.

“Kuna mabao ndani ya soka yanasisimua hata kama haupendi mpira utaupenda tu, wale wanaomkumbuka Ryan Giggs na Paul Scholes miaka ya 1980+ akiwa Man United mipira ikirudi kwenye ile semi cycle nje ya penati box (kale ka-nusu mduara) zile rebound alikuwa anapiga fimbo kama zile”-Mwl. Alex Kashasha.

“Ile inaitwa semi-breakway ni mpira ambao ameupiga sio juu ya anapofungia kamba za viatu lakini ni pembeni kidogo akafunguka yule bwana mdogo mpira mmoja mzuri sana.”

“Low range, kama ni kupima kwa kipimio basi nafikiri ni kilometa 112 kwa saa (112kph).”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here