Home Uncategorized Alliance Fc”Tupo Iringa tunasaka madini ya kuwabomoa matajiri wa Mbeya City”

Alliance Fc”Tupo Iringa tunasaka madini ya kuwabomoa matajiri wa Mbeya City”

6884
0

Baada ya matokeo hafifu klabu ya Alliance kupitia msemaji wake Mwafulango Lucas wameelezea maandalizi yao ya mchezo unaokuja dhidi ya mbeya City.

“Tuko mkoani Iringa, tukiendelea na maandalizi ya kucheza mchezo wetu unaofata wa ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya timu ya soka ya Mbeya city”

Ratiba za mtanange huo

Mchezo utakaochezwa kwanzia majira ya saa nane kamili za mchana siku ya Jumapili ndani ya uwanja wa Sokoine.

Benchi la ufundi la lipoje?

“Bado tuna imani na benchi la ufundi chini ya kocha mkuu MBWANA MAKATA, kocha msaidizi RENATUS MAYUNGA SHIJA, na KESSY MZIRAY, daktari wa timu ni ABEL SHINDIKA, na mtunza vifaa ni JOSEPHAT MUNGE, na benchi zima la ufundi kama nilivyosema”

Licha klabu hiyo kupata matokeo mabaya msemaji huyo amezidi kuwatia hamasa mashabiki na wadau wa soka kuwa bado klabu yao ipo sawa.

“Tuna imani kubwa na wachezaji wetu. Nasi kama uongozi tumejipanga ndio maana tumeamua kwa dhati timu kubaki mkoani Iringa tayari kujiandaa na mchezo wenyewe”

Kwanini mpaka sasa wapo mkoani Iringa? Je kuma siri gani kubwa?,

“Tunafahamu hali ya hewa ya mkoa wa Iringa na Mbeya inaendana kwa kila kitu. Kwahiyo tunajiandaa kikamilifu kuelekea mchezo huo”

Kocha mkuu wa klabu nae ana yapi?

“kocha anaendelea kuweka mbinu zake, anaweka madini ya kutosha kuelekea mchezo huo. Tunaamini vijana watayashika mafunzo ya mwalimu kwa ufasaha”

Vipi kuhusu safari yao kwenda Jijini Mbeya?

“Timu itaondoka hapa siku ya Jumamosi asubuhi kabisa kuwahi mkoani Mbeya, kuwahi kuwavaa matajiri wa jiji siku ya Jumapili”

Je kuna taarifa zozote za majeruhi? Vipi hali ya kipa wao tegemezi?

“Kikosi chetu hakina majeruhi wengi. Mchezaji ambaye anaweza kuukosa mchezo huo kutokana na hali ya majeruhi ni golikipa Kelvin Richard. Hata hivyo tunafurahi kumuona amerudi na ameanza mazoezi hivi sasa. Daktari wa timu amemthibitishia mwalimu anaweza kumtumia katika mchezo unaofata. Itakuwa maamuzi ya Mwalimu kumtumia au kutokumtumia”

Wanaonaje hali ya wachezaji wao kimchezo na kisaikolojia?

“Wachezaji wetu wako fiti kuivaa timu ya soka ya Mbeya city siku ya tarehe 16, na tuna uhitaji mkubwa wa alama tatu”

Wao wana mtazamo gani kwa wapinzani wao?

“Tunafahamu Mbeya city walipoteza michezo yao mitatu, na sisi tumepoteza michezo miwili tukitoka sare mchezo mmoja”

“Tunafahamu kila timu inaingia uwanjani ikitafuta matokeo katika mchezo huo. Lakini tunaamini timu iliyojiandaa vizuri itaweza kucheza vizuri katika mchezo huo”

Neno kwa mashabiki wao wa mkoa wa Mwanza na popote pale?

“Kikubwa niwatoe hofu mashabiki wa Alliance football klabu, popote walipo kwamba timu yao inaendelea vizuri na tunaendelea kujiimarisha vizuri katika kila idara kuelekea mchezo huo. Tuwaombe tu waendelee kutusupoti, waendelee kutuombea”

Mikakati mingine ya timu kwa sasa?

“Kuna utaratibu niliokuwa nimejiwekea, kwamba kocha mkuu, na nahodha mkuu mtawasikia siku ya Ijumaa mapema kabisa. Watatoa taarifa zao na mawazo yao kuelekea mchezo wenyewe siku ya Jumapili.

Ratiba za mazoezi yapoje?

“Kwa sasa tunamuachia Mwalimu na wachezaji kuendelea kuendeleza mikakati yao. Timu ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku. Asubuhi na jioni. Na inafanya mazoezi kwa kuelekea mchezo wenyewe wa Jumapili. Kwahiyo ningependa niwajulishe tu kinachoendelea katika kambi yetu ya Alliance football klabu, kwamba hali ni shwari, hali iko vizuri, wachezaji wana morali, wana shauku kubwa, wana hamasa kubwa, wana kimuhemuhe kikubwa kuelekea mchezo huo.

Pia wanazidi kuwakumbusha mashabiki wao kwamba?

“Ni maombi yenu, sala zenu, hasa nyinyi mashabiki wa Alliance football klabu. Na sisi pia tunajiombea na kuendelea kuomba kila siku. Hata wenzetu pia wanaomba. Lakini yule ambaye ameomba vizuri na kujiandaa vizuri anaweza kupata matokeo siku ya Jumapili. Kwaiyo nitangulize kusema kwamba, tutaendelea kupambana ili tutoke sehemu tuliyopo. Tunaamini tupo sehemu ambayo si nzuri na ndomaana tunaendelea kupambana.”


Majina yangu ni Luka Mwaflango wa idara ya habari ya mawasiliano ya Alliance football club.


Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here