Home Kitaifa Alliance inatafuta rekodi muhimu Shinyanga

Alliance inatafuta rekodi muhimu Shinyanga

4089
0

Alliance FC leo itakuwa ugenini ikitafuta rekodi moja tu itakapocheza dhidi ya Stand United ‘Chama la Wana’ kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Rekodi inayotafutwa na Alliance ni kushinda mechi ya kwanza ugenini au angalau kufunga goli ugenini, tangu wamepanda daraja kucheza ligi kuu wameshacheza mechi 8 ugenini lakini wamepata pointi moja tu, mechi 7 zilizobaki ilikula kwao.

TZ Prisons 2-0 Alliance
Mbeya City 2-0  Alliance
Lipuli 1-0 Alliance
JKT Tanzania 0-0 Alliance
Yanga 3-0 Alliance
Simba 5-0 Alliance
Kagera Sugar 1-0 Alliance
Mwadui 4-0 Alliance
Stand United ?? Alliance

Kocha msaidizi wa Alliance Kessy Mziray amezungumzia maandalizi yao kabla ya mechi dhidi ya Stand United na anakiri timu yake haijawahi kuonja ladha ya ushindi wa ugenini.

“Kadiri timu inavyocheza ndio inazidi kuimarika na kubadilika, hatujawahi kucheza ugenini na kushinda lakini tunashukuru tuliweza kushinda kwenyenmchezo wa FA Cup tena kwa magoli mengi ambayo hatujawahi kufunga.”

“Timu inavyozidi kuimarika hata sisi benchi la ufundi inatupa matumaini, tunaimani vijana wakitimiza majukumu tuliyowapa kwa mara ya kwanza tutaweza kuondoka na pointi tatu kwenye uwanja wa Kambarage.”

Alliance imeshinda mechi 4 kati ya 17 ilizocheza msimu huu, mechi zote imeshinda ikiwa uwanja wa nyumbani (Mwanza) itaweza kushinda kwa ugenini kwa mara ya kwanza?

🏟Mechi inachezwa uwanja wa Kambarage, Shinyanga
🕓Kuanzia saa 10:00 jioni.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here