Home breaking news Alliance yamtimua kocha mkuu, Kiungo wa Madrid kwenda darajani kwa mkopo

Alliance yamtimua kocha mkuu, Kiungo wa Madrid kwenda darajani kwa mkopo

11512
0

Aliyetangazwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Alliance ya Mwanza Baptiste Kayiranga, ameachana na timu hiyo baada ya kutaka kupunguza mshahara wake na kutaka afundishe pia timu ya wanawake ya Alliance. Tayari mkataba umevunjwa Kati ya Alliance, na kocha huyo kwa sasa Alliance, haina kocha mkuu.

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Lucas Perez, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Westham United, kwa mkopo.

Klabu ya Chelsea, imempiga faini goli kipa wao Thibaus Courtois, kiasi cha paundi 20,0000 kwa kosa la kukosa mazoezi na timu yake kujiandaa na msimu upya wa ligi kuu England 2018/19. Courtois, ambaye amekuwa akihusishwa kuondoka klabu ya Chelsea na kujiunga na klabu ya Real Madrid . Courtois, mwenye umri wa miaka 26 amebakiza mkataba wa mwaka moja ndani ya klabu ya Chelsea.

Klabu ya Real Madrid, ipo tayari kumtoa Mateo Kovacic, kwenda klabu ya Chelsea kwa mkopo. Kovacic, ambaye hivi karibuni ameomba kuondoka katika klabu ya Real Madrid, na kujiunga na klabu kadhaa zikiwemo Inter Milan, na Manchester City, zilikuwa zikimuwania mchezaji huyo. Hata hivyo klabu ya Real Madrid aipo tayari kuumuza kiungo huyo. Makubaliano baina ya Chelsea, na Real Madrid, zitatangazwa baada ya masaa 48 yajayo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here