Home Ligi Kuu Bara Alliance yatamba kulitikisa jiji la Mbeya, yatoa onyo kwa askari magereza

Alliance yatamba kulitikisa jiji la Mbeya, yatoa onyo kwa askari magereza

7863
0

Klabu ya Alliance imesafiri kilometa 909 ambapo ni mwendo wa saa 15 na dakika 8 mpaka jiji la Mbeya kwa ajili ya mpambano wao dhidi ya Tanzania Prisons.

Klabu ya Alliance imeweka kambi Mbeya mjini ikiwa na wachezaji 24. Kila mchezaji na kiongozi wa timu wana morali na nia kubwa ya kutafuta alama 3 za muhimu. Utakuwa mchezo wa aina yake hasa kutokana na pande zote kuwa na uchu wa kupata ushindi wao wa kwanza wa ligi kuu msimu huu.

Tz Prisons ndio kwanza hawana alama hata moja na watawakaribisha Alliance ambao bado hawajaonja ladha ya ushindi tokea klabu hiyo ianzishwe.

Mpaka sasa klabu ya Alliance haijaonja ushindi tokea wamepanda ligi kuu kwa mara yao ya kwanza. Hapo awali walipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya wapinzani wao Mbao Fc kabla ya kusubiria kwa dakika 181 kupata bao lao la kwanza ligi kuu kupitia kwa Michael Chinedu kwenye mtanange wao dhidi ya African Lyon katika mchezo uliokwenda sare ya 1-1.

Wanakwenda kukutana na Tanzania Prisons ambao mchezo wa wa mwisho walipata kichapo cha bao 1 kwa nunge kutoka kwa wakata miwa wa Mtibwa. Ikumbukwe mchezo wao wa awali Wajelajeala walipoteza mchezo wao kwa bao 1 bila majibu na mabingwa wa Tanzania bara msimu uliopita.


Alliance wamecheza michezo miwili nyumbani na kupata alama moja na bao moja huku wakiruhusu bao 1 pia.

Tanzania Prisons wamecheza michezo miwili yote ya ugenini na hajapata bao lolote lakini wameruhusu mabao mawili.


Msemaji wa Alliance Jackson Luka Mwafulango ameelezea dhamira ya klabu yake,

“Tunajua mchezo una matokeo matatu, tutakayoyapata ni matokeo ambayo Mwenyezi Mungu ametupangia. Mungu anakupa kile anachotaka yeye na siyo kile unachotaka wewe”

Mwafulango pia anaamini kuwaa uzoefu wanaoendelea kuupata Alliance ndio utakaoleta chachu ya wao kuendelea kupambana zaidi. Anaamini kiwa kila mchezo wanaocheza ni hatua muhimu kuelekea mchezo unaofuata.

“Alliance ni kama maji ya bomba. Unapozidi kuyafungua ndipo kasi inaongezeka zaidi. Kama ndugu zetu wakitufungua kwa spidi basi watambue kuwa kasi yetu ya maji sio ya kawaida. Lakini sisi tutajitahidi kuhakikisha kasi yetu inakuwa kubwa kidogo”


Hili litakuwa jaribio lao la kwanza wakiwa nje ya jiji lao. Wamecheza michezo miwili ya mwanzo wakiwa na msaada mkubwa wa mashabiki wake wa nyumbani. Lakini mwafulango bado amewasihi mashabiki wa Alliance waliopo Mbeya na hata wale wenyeji la Mwanza basi wajitokeze kuisapoti timu yao.

“Kama wewe ni shabiki wa Alliance popote ulipo tunakuomba utuunge mkono nasi tutapata ushindi kwa niaba yako”

Alliance licha ya ugeni wao bado wanaamini safari hii moto wao hautazimwa hata kidogo. Wamejianda vilivyo na imani yao kubwa ni kuonesha uwezo wao ulivyo madhubuti.

“Tunawaomba mashabiki watusapoti sana, sio kwa mchezo wa Prisons pekee ila na michezo mingine inayokuja. Sisi tumejiandaa vilivyo”

Ratiba

Septemba 1, 2018
› Ligi Kuu Bara
Stand U. 9:00 Biashara Mara United
Coastal Union 9:00 Kinondoni MC
Mtibwa Sugar 9:00 Mbeya City
Kagera Sugar 9:00 African Lyon
Tanzania Prisons 9:00 Alliance
Simba Haipo Lipuli
Azam Haipo Ruvu Shooting

Taarifa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here