Home Kimataifa Amri Kiemba aipa ubingwa wa ligi kuu Tanzania timu hii

Amri Kiemba aipa ubingwa wa ligi kuu Tanzania timu hii

11917
0

Wakati ligi kuu Tanzania bara ikitarajia kuanza Jumatano hii baada ya pazia lake kufunguliwa rasmi siku ya Jumamosi iliyopita kwa mchezo wa Ngao ya Jamii, mchezaji wa zamani wa ligi hiyo Amri Kiemba ametaja timu yenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Mbali ya kuitaja timu hiyo, Kiemba pia amezungumzia mtazamo wake kuelekea ligi kuu msimu huu.

“Kwa maandalizi ya timu hadi sasa naona Simba wana maandalizi mazuri kwa kujaribu kuziba mapengo yaliyokuwepo msimu uliopita pia wameendelea kukitunza kikosi walichokuwanacho msimu uliopita.

Kwa hiyo nadhani wana nafasi nzuri ya kuweza kuchukua ubingwa msimu huu unaokwenda kuanza lakini pia nina wapa nafasi Azam kwa sababu ya timu yao walivyoitengeneza, ina muunganiko wa vijana wengi na baadhi ya wenye uzoefu. Msimu uliopita walikuwa wanapita kwenye transition ya kurekebisha timu lakini msimu huu watakakuwa tayari kwa kushindana.

Pia Yanga hauwezi kuwatoa kutokana na ukubwa wao kwenye ligi japo na wao wapo kwenye transition ya kutengeneza kikosi kutoka kwenye kile ambacho kilikuwa kinawapa ubingwa kwenye misimu mitatu iliyopita na kutengeneza kikosi kipya ambacho kitashindana.

Siwatoi kwenye mbio kwa sababu ya uzoefu walionao kama klabu kwenye ligi yetu, lakini katika uhalisia watakuwepo kwenye mapambano lakini siwapi nafasi ya kuchukua ubingwa.”

Timu zilizopanda daraja msimu huu (African Lyon, KMC, JKT Tanzania, Coastal Union, Biashara pamoja na Alliance) ipi itatisha?

“Kwa nilivyowaona KMC nadhani watakuwa washindani wazuri kwenyd ligi kwa sababu wana muunganiko wa wachezaji vijana na wazoefu na wanamwalimu ambaye anaamini kwenye kile ambacho amekisomea. Nadhani wanaweza kufanya vizuri kama timu sio mchezaji mmoja-mmoja”

Zitakazoshuka daraja.

“Kusema timu itashuka daraja ni ngumu kwa sababu timu inapanda ligi kuja kushindana na wenyewe wameshaona mapungufu waliyonayo nadhani ambaye hakujiandaa vizuri atakuwa amejitengenezea mazingira ya kuteremka hata kama alikuwepo kwenye msimu uliopita.”

Kuhusu mfungaji bora.

Nadhani mfungaji bora wa msimu uliopita (Emanuel Okwi) anaweza kuendelea kupigania lakini pia wanaweza kuibuka watu wengine ambao watam-challenge kutokana na ujio wa washambuliaji wapya kama Kagere, Makambo, lakini itategemea na perfomance ya timu kwa sababu mchezaji anategemea timu ina-perform vipi na kumpa support kufikia malengo ya kuwa mfungaji bora.

Ongezeko la wachezaji wa kigeni vipi?

“Kuongezeka kwa wachezaji wa kigeni inaleta changamoto kwa wachezaji wazawa lakini wachezaji gani ambao wanaongezwa hilo ni jambo jingine kwa sababu kama unamleta mchezaji ambaye anakuja kukaa nje kwenyd timu yako si dhani kama ni changamoto kwa waliopo zaidi ya kujiongezea mzigo wa kulipa wachezaji wa kigeni. Watu wazingatie wachezaji wanaokuja wawe ambao wanathaminika na wanashiriki kwenye michezo ya kimataifa kwenye nchi zao, hao wataleta chachu kwa wachezaji wa ndani”

Timu 16 hadi 20 kwenye ligi

Kukua kwa soka hakutegemei ligi ina timu ngapi bali ni kuiboresha ligi yenyewe. Timu zipo 20 lakini si dhani kama ligi tuliyoiona msimu uliopita ambapo Majimaji walikuwa wanakwenda kucheza huku hawajui mchana watakula nini halafu tunaongeza tena timu nyingine za aina hiyo.

Nadhani iwekwe sheria au kanuni, timu yenye mtaji wa kiasi fulani ndiyo inastahili kucheza ligi kuu sio kila timu icheze ligi kuu nadhani itasaidia kukabiliana na ukata kwenye tumu za ligi kuu.

Ligi kukosa mdhamini.

Tumezoea kwamba, mdhamini mkuu wa ligi ndio anaziwezesha timu. Kukosekana kwa mdhamini kunaweza kuchangia kupunguza ushindabi lakini pia iwe ni somo kwa vilabu kwamba kila klabu inatakiwa kutafuta wadhamini wa kuiwezesha kushindana kwenye ligi bila kutegemea mdhamini mkuu wa ligi.

Kila timu ingekuwa na watu wa masoko wanaoweza kutafuta watu wa kuwasaidia kuendesha timu, tili yetu ingekua bora zaidi kuliko hivi ambavyo wanategemea mdhamini mkuu ndio awawezeshe kwa kila kitu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here