Home Kimataifa Andrew Robertson ana mioyo miwili akiwa Uwanjani

Andrew Robertson ana mioyo miwili akiwa Uwanjani

6021
0

Robertson ni silaha ya Liverpool yenye mioyo miwili. Moyo wa kwanza unatumika kipindi cha kwanza, na moyo mwingine unatumika kipindi cha pili. Ule upande ambao anacheza Mane na Robertson, bila shaka ni upande ambao kocha Jurgen Klopp anautegemea sana.

Umewahi kuona ule upande unavujisha magoli ya kizembe? Umewahi kuona mapungufu yanaonekana dhahiri upande ule? Jibu ni hapana. Ule upande ni imara sana kwa sababu Sadio Mane hamchoshi Robertson, na Robertson hamchoshi Mane.

Wakati Liverpool hawana mpira, Unamuona Mane anaongeza mchango wa ulinzi pia hata Robertson anamsaidia Mane kushambulia. Robertson sio beki tu ila hata kushambulia yumo. Kasi yake anayoanza nayo kipindi cha kwanza huwa ni ileile anayorudi nayo kipindi cha pili. Hachoshi kumtazama, anatoa kila kitu alichonacho kwaajili ya timu. Ni moja kati ya wachezaji ambao hawakuangushi uwanjani.


Penati aliyofunga Mohamed Salah, inamaanisha kwamba timu hizi mbili za Arsenal na Liverpool, zimefungana idadi ya magoli mengi zaidi (154) kwenye historia ya mashindano.


Ndio maana ameshahusika kwenye kutengeneza nafasi kumi za kufunga magoli. Anajua kuisukuma Liverpool pale inapotakiwa kufika. Anacheza kwa hisia, haogopi hata kidogo. Naamini unaweza kuona utafauti wa upande wa anaocheza Salah na Trent- Aleksandar Anold na upande wa kulia anaocheza Robertson pamoja na Sadio Mane.

Wanapocheza akina Robertson Mane, inaonekana pana udhabiti wa hali ya juu kwasababu wote wanazuia na kushambulia kwa pamoja. Robertson sio sawa na jiko la gesi ambalo linahitaji uwe unapunguza moto na kuongeza. Ukiwasha umewasha, hakuna hofu unayokutana nayo kwa muda wote wa dakika tisini za mchezo

Bado ana miaka 24, maana yake bado damu ni changa. Ana sifa kuiongoza timu uwanjani, ndomaana amepewa kitambaa cha unahodha kule kwenye Taifa lake la Scotland. Nategemea kumuona siku moja akipewa majukumu ya kuiongoza Liverpool akiwa nahodha. Wachezaji wanaojitoa asilimia mia moja, wanafaa kuwa viongozi sababu wanakuwa na uchungu na timu.


Roberto Firmino mpaka sasa ameifunga Arsenal magoli 7 na kutoa assist 3, jumla magoli (10)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here