Home Kimataifa Arsenal kutia mchanga kitumbua cha Klopp?

Arsenal kutia mchanga kitumbua cha Klopp?

5291
0

Leo ndio leo, ni Liverpool dhidi ya Arsenal, itakayoanza saa 2:30 usiku. Mchezo wa 227 kati ya Liverpool na Arsenal kwenye mashindano yote. Liverpool wameibuka vidume katika mechi zao kwa kushinda mara 86 wakati Arsenal imeshinda mara 79. Timu zote zimegawana alama mara 61.


Nimetimiza ndoto yangu baada ya kupata nafasi ya kucheza Arsenal, lakini ili nizidi kufurahia ndoto yangu natamani sana leo tuifunge Liverpool


Arsenal hawajashinda kwenye mechi zao tano zilizopita ambazo wamesafiri kwenda Anfield kukutana na Liverpool kwenye Ligi Kuu England. Wametoa sare (2 na wamepoteza mechi 3)


Unai Emery, anatarajia kuona kama kuna uwezekano wa  Shkodran Mustafi, kuanza leo baada ya kupata matatizo ya nyama za paja.

Wachezaji wengine ambao mwalimu ana wasiwasi juu ya uwezo wao kucheza ni Nacho Monreal (nyama za paja) and Emile Smith Rowe (kiuno)

Wachezaji ambao hawatakuwepo kabisa ni Hector Bellerin (kifundo), Konstantinos Mavropanos(kiuno), Rob Holding (goti), Henrikh Mkhitaryan (mguu) and Danny Welbeck (kifundo)

Mesut Ozil amemwambia meneja kuwa hawezi kucheza mchezo wa leo kwa sababu anasikia maumivu ya goti


Liverpool wamecheza mechi 7 bila kupoteza dhidi ya Arsenal kwenye mashindano yote( wameshinda mechi 3 na sare 4)

Kumekuwa na magoli 149 kwenye Ligi Kuu England kati ya Liverpool na Arsenal. Ni ratiba ya mechi nne tu imefikisha magoli 150 kwenye mashindano( Arsenal Vs Everton, Liverpool Vs Tottenham, Chelsea vs Tottenham na Arsenal Vs Tottenham.

Arsenal wamefunga magoli mengi zaidi( 9)kutoka nje ya box la timu pinzani kuliko timu yoyote msimu huu, wakati Liverpool imebaki timu pekee ambayo bado haijafungwa goli kutoka nje ya box msimu huu 2018/2019

Arsenal wameshinda mechi moja kati ya 12 za ugenini walizocheza na Liverpool

Liverpool wameruhusu magoli Saba kwenye mechi 19 za Ligi Kuu England msimu huu, na endapo hawataruhusu goli kwenye mechi ya kesho itakuwa rekodi ya kuruhusu magoli machache katika mechi 20 za Ligi Kuu.

Mshambiliaji wa Liverpool Roberto Firmino amehusika kwenye magoli nane katika mechi sita zilizopita dhidi ya Arsenal( magoli 5, Assist 3) Ni Robbie Fowler tu ndiye amefunga magoli mengi zaidi (9) dhidi ya Arsenal kuliko Firmino ambaye amefunga magoli (5)

Mshambuliaji wa Arsenal Piere Aubameyang ndiye anaongoza kufunga magoli mengi kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Amefunga magoli 13. Aubameyang amefunga magoli 6 kwenye mechi nane zilizopita za ugenini.

Makamu nahodha James Milner lakini Alberto Moreno ameanza mazoezi mepesi. Wachezaji wengine ambao hawatakuwepo ni Dominic Solanke ana shida ya misuli Joe Gomez  hatakuwepo na Joel Matip pia nae hatakuwepo

“Milner hayupo kabisa leo labda mchezo ujao,” Klopp

Pos Team P GD Pts
1 Liverpool 19 36 51
2 Tottenham Hotspur 19 24 45
3 Manchester City 19 36 44
4 Chelsea 19 21 40
5 Arsenal 19 16 38
6 Manchester United 19 6 32

Vikosi vya mwisho : Liverpool v Newcastle (Dec 26): Alisson, Alexander-Arnold, Lovren, Van Dijk, Robertson, Henderson, Wijnaldum, Shaqiri, Firmino, Mane, Salah.

Brighton v Arsenal (Dec 26): Leno, Lichtsteiner, Sokratis, Koscielny, Kolasinac, Xhaka, Torreira, Guendouzi, Ozil, Lacazette, Aubameyang.

@Patrick Admila

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here