Home Ligi EPL Asian Games 18, Japan washikilia tiketi ya Heung Min Son kwenda au...

Asian Games 18, Japan washikilia tiketi ya Heung Min Son kwenda au kulikwepa jeshi

10284
0

Timu ya taifa ya ya Japan imeibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Falme za Kiarabu katika michuano ya bara la Asia inaoyoendelea huko Indonesia hivi sasa.

Kwa matokeo haya sasa Japan wanakwenda kukutana na timu ya taifa ya Korea Kusini ambao wenyewe wamefudhu fainali kwa kuitoa Vietnam kwa mabao 3-1.

Ikumbukwe kwamba nyota wa Tottenham Hotspur Heung Min Son baada ya timu ya taifa kufanya vibaya katika kombe la dunia alipaswa kwenda jeshini kutokana na kuwa na umri ambao anatakiwa aende jeshini(26).

Kwa nchi ya Korea Kusini kama mwanamichezo hajaifanyia nchi yake kitu kikubwa itambidi aende jeshi miezi 21 kama raia wa kawaida kabla ya kufikisha miaka 28 na Heung alikuwa moja ya wanasoka wanaosubiria kulitumikia jeshi.

Lakini sasa matumaini ya Heung kutoenda jeshini yamefufuka kwani kama nyota huyo watafanikiwa kuifunga Japan siku ya Jumamosi baasi ataendelea na majukumu yake katika klabu ya Tottenham na hatakwenda jeshini.

Lakini endapo Korea Kusini watakubali kipigo kutoka kwa Japan katika mchezo huo baasi nyora huyo itabidi aende kulitumikia jeshi lao.

Kabla ya mchezo wao dhidi Vietnam wameanza kumtania Son kwa kubeba mabango yenye picha yake akiwa jeshini wakimaanisha kwamba nyota huyo atapoteza dhidi yao na atakwenda jeshini.

Tayari Son amefeli katika michuano ya Olypmpic 2016 kuisaidia Korea, akafeli tena Urusi na hii sasa ya Asian Games ndio nafasi pekee kwake iliyobaki kujiokoa na jeshi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here