Home Kimataifa Baada ya mechi 4 tu, Cr7 aanza madai mapya Juventus

Baada ya mechi 4 tu, Cr7 aanza madai mapya Juventus

13087
0

Kuishi na jogoo ni tofauti na kuishi na kifaranga, hilo utaliamini ukianza kufuatilia maisha ya nyota mpya wa Juventus Cristiano Ronaldo ambaye amehamia msimu huu akitokea Real Madrid.

Tangu aanze kuichezea Juventus katika Serie A ameshacheza michezo minne, lakini katika michezo hiyo mchezaji huyo wa Ureno hajawahi kufunga goli hata moja katika klabu yake hiyo mpya.

Jarida la Forza Italian limesema Cristiano Ronaldo amewaomba Juve kuangalia namna ambayo familia yake inaweza kulindwa zaidi ya inavyolindwa hivi sasa.

Kwa hali ilivyo sasa ambapo Ronaldo amekuwa habari kubwa sana inaifanya faimilia yake kuangaliwa sana na watu kutamani kuwaona na hata kujua wanapoishi.

Hii imemfanya Cr7 kuwaambia Juventus watafute namna ambayo mpenzi wake na watoto wake watakuwa wanapewa ulinzi zaidi kila mahali ambapo watakuwa wanakwenda.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here