Home Kimataifa Balotelli anarudi England kutaga au kuwika?

Balotelli anarudi England kutaga au kuwika?

8466
0

Jinsi akili yake ilivyokuwa makini katika kufunga, alionekana kama angekuwa Andy Shevchenko mpya katika sura nyeusi. Hata katika miguu yake alionekana kuwa na kila kitu ambacho mshambuliaji namba tisa anatakiwa awe nacho. Katika umri wake mdogo kila mtu alitamani kumjua Balotelli ni nani. Kila muda ulivyozidi kwenda magoli yalimpenda haswa.

Alipata nafasi ya kubwa sana masikionj mwa wengi akiwa na umri mdogo. Ndani ya klabu ya Inter Milan alionyesha dunia kuwa yeye ni nani. Kila mtu leo anakumbukumbu jinsi alivyocheka na nyavu pale San sirro chini ya kocha mtukutu Jose Mourinho. Ingawa Mourinho na Baloteli ilikuwa sawa kuchanganya bangi na ugoro.

Balotelli alikuwa na vipaji viwili, kipaji cha kufumania nyavu na kipaji kiburi na utukutu. Kutoka na utovu wa nidhamu kipaji chake kilianza kuonekana kama taa kwenye mchana wenye jua la kutosha.

Alishindikana. Yamkini Roberto Mancini ndiye mwanadamu aliyemvumilia Balotelli. Binafsi yake aliamini Baloteli kuna siku ataishi atajitambua na kuweka heshima kwenye dunia hii ya Messi na Ronaldo. Mwaka 2010 alimchukua na kumleta katika klabu ya Man city.

Alimpa alichokitaka na alichostahili kupata. Baloteli aliishi kama Mabuto Seseko kwa mshahara mzuri, nafasi uwanjani ili tu afanye kile ambacho mifupa yake imeumbwa kufanya. Usoni mwa Baloteli, Mancini aliona sura ya Fernando Torres. Sisi huku tulimuona kama pete ya dhahabu kwenye pua ya Nguruwe.

Mancini aliamini Balotelli alikuwa zaidi maskini akampa mshahara mnono, lakoni alisahau rangi ya Baloteli sio nyeusi ili ni utukutu.

Baloteli alipofika alifanya kila alichoona kwake sawa. Hakumjali Roberto Mancini wala babu yake Mancini. Uzuri ni kwamba ukiachia rangi yake ya utukutu, lakini seli zake za damu bado zilijaa hari ya kufunga magoli.

Akaenda Milan. Waroma wanakwambia akazaliwa upya ingawa sikumbuki ni Mathayo ngapi. Taratibu akabadilika na kuwa mtu wa busara. Labda kwa sababu kwenye majukwaa ya Milan alikuwa akimuona kipenzi chake mama yake mlezi wa kitaliano Silvio Balotelli.

Bila shaka angekuwa mjinga na hata mlango wa mbinguni angeusikia tu. Si sheria za dini anayoiabudu zinasema waheshimu wazazi? Ndio, alifanya hivyo. Hata alipobaguliwa hakupigana na mtu, alilia, akaamua kutoka nje.

Paundi milioni kumi na sita zikampeleka zikamleta tena Anfield mwaka 2014. Ni taifa lile lile ambao waandishi wa habari waligeuka kuwa nzi na kumfanya Baloteli kama kinyesi.

Kila mara walimfuata kumhoji ilo tu wapate kiki kwenye kurasa magazeti yao. Wakati huu nadhani angekuwa maarufu kwenye magazeti kuliko hata David Cameroon.

Ni kama Liverpool walimfanya Herode kuwa mkombozi wao. Wakaamini kuwa maisha ya Liverpool yatamfaa. Wapo waliodhania Robbie flower amerudi. Tehe tehe.

Baloteli ni Balotelli tu. Mwingine fotokopi. Alorudia tabia yake ambayo ilimpelekea yeye kufunga goli moja tu. Mwisho akakimbilia zake Ufaransa ambapo hata akinya pale kwenye mnara mkubwa wa Paris magazeti hayatamfuatilia yeye ila yataandika gharama za nywele za Neymar.

Kwa mara nyingine anataka kurudi England akacheze Newcastle. Ni baada ya kushindwana na kocha wake Patrick Vieira katika klabu ya Nice. Bado ana umri wa miaka 28 dunia haimuwazi tena. Kwa lipi?

Hamna. ni Mancini tu aliyekubali kujifungia kwenye gereza la ndoto zake akiamini kuwa nidhamu ni sawa ukuta ukipaka rangi tu unang’aa. Tuone akija England anakuja kufanya nini, kuwika au kutaga.

Na MESHACK MELELE

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here