Home Ligi EPL Barcelona wanavyotumia mbinu walizomnasia Coutinho kumpata Pogba

Barcelona wanavyotumia mbinu walizomnasia Coutinho kumpata Pogba

12061
0

Ndani ya wiki moja tayari nyota wawili wa Barcelona wamemzungumzia kiungo wa Manchester United Paul Pogba pasipo hata kutarajia.

Alianza Gerrard Pique ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alisema kwamba amgefurahi sana kama angemuona Paul Pogba akiwa ndani ya uzi wa Barcelona hivi karibuni.

Lakini wakati mashabiki wa Manchester United wakijaribu kujisahaulisha kuhusu comment ya Pique, Luis Suarez naye huyu hapa ameibuka na la kwake kuhusu Paul Pogba.

Akizungumza katika kituo kimoja cha redio mjini Catalunya aliulizwa kuhusu tetesi za Paul Pogba kujiunga na klabu ya Barcelona katika dirisha lijalo la usajili.

Suarez amesema Paul Pogba ni mchezaji wa daraja la dunia na ameshashinda karibia kila kitu lakini ni mchezaji wa Manchester United, lakini Suarez akasisitiza kwamba nyota huyo anakaribishwa Barcelona akitaka kwenda.

Kama unakumbuka Barca hawa hawa wakati wanamtaka Coutinho walikuwa wanamuongelea sana, Paulinho, Messi pamoja na wachezaji wa zamani akiwemo Rivaldo na Xavi walikuwa kila siku wakisema wanatamani kumuona Coutinho akiwa Batcelona.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here