Home Kitaifa Bingwa wa TPL atapata nini?

Bingwa wa TPL atapata nini?

7911
0

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limekiri kwamba hadi sasa haijulikani bingwa wa ligi kuu Tanzania bara atapata zawadi gani baada ya aliyekuwa mdhamini mkuu wa ligi hiyo kujiweka pembeni hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema, pamoja na hayo TFF bado ipo kwenye mazungumzo na makampuni mbalimbali nchini kuhakikisha kwamba bingwa anapata zawadi inayostahili kulingana na ligi husika.

Baada ya kusema ligi inaanza bila udhamini, mdhamini amejiondoa kuna vitu vingi bado vinafanyiwa kazi na Vodacom kabla ya taarifa rasmi kutoka kama wataendelea au hawatoendelea lakinini bado tupo kwenye majadiliano makubwa.

Bado tubajadiliana na makampuni mengi kwa ajili ya kupata co-sponsors wengi ambao ukiwaunganisha wanaweza kutengeneza thamani kubwa ya ligi. Ni vitu ambavyo vinafanyika kwa nguvu kubwa .

Vingozi wa taasisi na mimi hatulali tunafanya kazi kubwa kubwa kuhakikisha mzunguko wa ligi wa raundi ya 6, 7 au 8 tunapata mdhamini mkuu lakini kupata co-sponsors ni kitu kikubwa zaidi kwa sababu tutapata watu wadogowadogo lakini wengi ligi itakuwa na thamani kubwa.

Ni vyema tuipe thamani ligi yetuinawezekana tunapita kipindi kigumu lakini mwisho wa siku thamani ya ligi itaonekana. :
Kuhusu bingwa atapewa nini mshindi wa pili na watatu na zawadi nyingine ni kitu tofauti, tutakapokuwa tumepata mdhamini mkuu na wadhamini wenza tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujua bingwa atapata kitu gani kwa sababu kati ya proposal tulizokuwa tunapeleka zimekuwa zinaonesha kiwango ambacho bingwa anapaswa kupata kwa maana ya kuongoza kiasi ambacho anapaswa kupata bingwa.

Hatuwezi kusema bingwa atapata nini hadi pale tutakapokuwa tumekubaliana na mdhamini juu ya yale tuliyoyaainisha kama sehemu ya udhamini wa ligi kuu. :
Inawezekana mazungumzo yakashindikana kwa mdhamini mmoja lakini bado haimaanishi ligi itachezwa bila mdhamini mpaka mwisho. Tumekuwa tukifanyia kazi hili jambo kwa kiwango kikubwa, tuna watu wengi ambao tunafanya nao mazungumzo. Tunaendelea kulinda thamani ya ligi yetu kwa kiwango ambacho ligi yetu inapaswa kuwa inadhaminiwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here