Home Kitaifa Bocco matumaini kibao Simba vs AS Vita

Bocco matumaini kibao Simba vs AS Vita

2711
0

Kikosi cha Simba kimewasili leo jijini Dar es Salaam kikitokea Algeria kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi ambapo walipoteza mchezo huo kwa kufungwa na JS Saoura magoli 2-0.

Baada ya kutua Dar, nahodha wa timu hiyo John Bocco amesema anaamini marekebisho atakayofanya mwalimu na maandalizi anaamini watashinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya AS Vita na kufuzu hatua ya robo fainali.

“Haikuwa malengo yetu kupoteza mchezo dhidi ya Saoura lakini ndio sehemu ya mchezo. Tumerudi nyumbani tuna mchezo mwingine tutacheza na AS Vita mchezo ambao utaamua kama tutavuka kwenda robo fainali”-John Bocco, nahodha Simba.

“Kwa morali ya wachezaji na mbinu za kocha tukiwa kwenye uwanja wa nyumbani naamini tutashinda na kuvuka kwenda hatua ya robo fainali.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here