Home Kitaifa Bushiri amtimua Amri Said Mbao FC

Bushiri amtimua Amri Said Mbao FC

3725
0

Wakati jana Jose Mourinho akiachana na Manchester United, leo pia Amri Said ameachana na klabu ya Mbao FC ya Mwanza inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara.

Amri Said amekubaliana kuvunja mkataba na Mbao baada ya timu hiyo kumwajiri Ally Bushiri kama kocha msaidizi wa klabu hiyo.

Amri amesema hawezi kufanya kazi na Bushiri kwa sababu wote wana leseni sawa (leseni B ya shirikisho la soka Afrika-CAF). Amesema alikuwa tayari kuletewa kocha ambaye amemzidi daraja la leseni ili yeye awe msaidizi au angeletewa kocha mwenye daraja la chini yake lakini si ambaye wako daraja moja.

Amri tayari ameagana na wachezaji leo asubuhi kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza tayari kwa ajili ya kuanza maisha mapya.

“Siwezi kufanya kazi na Ally Bushiri kwa sababu walipaswa waje kabla hawajafanya nae mazungumzo kabla ya kumalizana nae, hata Bushiri alipaswa anipigie simu kama kocha aniambie viongozi wako wameniomba nije nikusaidie vipi hapo kuna mapungufu gani na hali ya kazi ipoje”-Amri Said.

“Lakini mambo yanapelekwa kwa njia za panya, ukishaona hivyo ujue kitu hicho hakipo sahihi. Kocha mwenye leseni C ningemkubali na nilipendekeza majina ya makocha ambao wamenizidi nipo tayari kufanya nae kazi.”

Amri Said anaiacha Mbao ikiwa katika nafasi ya nne (4) kwenye msimamo wa ligi baada ya kushinda mechi yao iliyopita dhidi ya Mwadui na kufikisha pointi 24.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here