Home Kitaifa Cannavaro “Sorry my friend”

Cannavaro “Sorry my friend”

11637
0

“Nadir Haroub ni mchezaji mwenye nidhamu ya hali ya juu. Nilipoulizwa kuhusu mchezaji gani naona anafaa kupewa kitambaa cha unahodha mwaka 2010 nilimtaja Cannavaro kutokana na heshima yake. Niliongea na viongozi na wakakubali” Maneno ya Abdi Kassim “Bab” Ballack wa Unguja.

Mapema siku ya jana wakati Cannavaro anaagwa, klabu ya Yanga ilitaka kustaafissha jezi namba 23 lakini yeye mwenyewe akaomba jezi ile apewe Shaibu Abdala Ninja. Kama ilivyokuwa kwa Bab kumkabidhi Nadir kitambaa, basi jana nae Nadir ameamua kumkabidhi jezi Ninja na viongozi wakakiri.

“Cannavaro atakumbukwa kwa mengi. Ni mchezaji mcheshi sana na ni mtu ambaye huwa hapendi kushindwa” Juma Kaseja

Tumemuona Cristiano Ronaldo katika umri wa miaka 34 amekuwa na kiwango bora, Tuliona Pia hata Zidane akiwa na zaidi ya miaka 30 alifanya makubwa, pia tumemuona Wayne Rooney jana akiisadia timu yake kupata mafanikio, vivyo hivyo Juma Kaseja anaamini kuwa kujitunza kwa Cannavaro kumemfanya awe katika kiwango chake bora.

Kaseja anaamini kuwa bado Cannvaro alikuwa na uwezo wakuendelea kucheza soka la kulipwa bila tatizo lolote.

“Cannavaro tokea awali alikuwa na nidhamu kubwa sana lakini hata hivyo namna umri wake unavyozidi kwenda alikuwa akicheza kwa utulivu mwingi na usalama zaidi kwa sababu tayari amekwisha pevuka kiakili na amekomaa kisoka zaidi lakini inabdi tu niheshimu maamuzi yake.

Nasema hivyo kwa sababu kuna kipindi tulicheza Simba na Yanga. Cannavaro alikuja kucheza penati ya mwisho lakini niliidaka. Kosa langu nilimrushia mpira usoni kitendo ambacho alikichukulia cha kawaida. Angekuwa mchezaji mwingine ungezuka ugomvi. Baadae nilikutana nae kambini timu ya taifa nikiwa na hofu kuwa hatutakuwa na mahusiano mazuri lakini aliponiona tu akanikumbushia lile tukio akiwa ananiambia “bwana bwana we jamaa weewe sio mtu mzuri kabisa” lakini hakuonesha kukasirrika wala hakuwa na chuki tuliishia kucheka tu” Juma Kaseja

“Mimi nadhani wengi hawatamuangalia kama mchezaji mzuri kwa sasa kwa sababu tu amezoeleka kwa kipindi kirefu akicheza hivyo hapo baadae Yanga watakuja kugundua ameondoka mchezaji mkubwa sana na aliyehitaji heshima ya kipekee” Juma Kaseja.

Kuhusu Nidhamu kaseja bado anasisitiza jukumu hili kwa waalimu wa vijana wadogo na wazazi kwa ujumla. Kwamba wanapaswa kuwalea watoto katika maisha ya kisoka zaidi

Kaseja anakubali kwamba Cannavaro alikuwa naa nidhamu yake yeye kama yeye. Anaamini kuwa alivyokuwa Cannavaro ndivyo alivyolelewa. Anashangaa kusikia watu wanahimiza watu wawe kama Cannavaro.

“Nidhamu ni malezi. Anavyoishi mchezaji amelelewa hivyo hivyo. Huwezi kumlazimisha Nyosso awe kama Cannavaro. Ataishi maisha feki.”

“kuna tofauti kubwa sana ya nidhamu ya uwanjani na nidhamu ya mtu kama alivyo. Watu wameshindwa kutofautisha maisha binafsi na maisha ya mchezaji ndani ya uwanja”

“Baloteli hawezi kuwa kama Ozil wala Messi hawezi kuwa kama Flamin”

“kikubwa ni kufuata maelekezo ya mwalimu, watu kama akina Bobban nimeishi nao sana, hana tatizo na mtu uwanjani, anawahi mazoezini kila mara alikuwa anajituma mazoezini mno lakini ukija kwenye magazeti utakuta yanamchafu kuwa ana nidhamu mbovu”

“angekuwa na nidhamu mbovu mwalimu asingemtumia. Nidhamu ya mchezaji ni kufanya alichotumwa na mwalimu na sio namna ya mtu kuongea au kucheka cheka na watu. Huwezi kumuiga mtu, huwezi utakuwa wa ajabu na tutajua tu kwamba unaishi maisha ya kuigiza” Juma Kaseja.

“Cannavaro hakuwa mzuri uwanjani tu pia alikuwa akipigania haki za wachezaji wake kwenye suala la maslahi na alikuwa na muono wa mbali. Anaifahamu Yanga kuanzia juu mpaka chini. Ni msikivu sana. Hajalishi anaambiwa na mdogo au mkubwa ila anaangalia faida ya jambo hilo”

“Nakumbuka sana kwa ucheshi wake. Siku moja tukiwa Misri na timu ya taifa alikosea chumba chetu aliporudi kutoka kuoga. Sasa wakati anarudi akaenda kugonga chumba kingine. Nilimsikia akiwa anaiita kwa kiswahili lakini sio mlango wetu. Nikawa nataka kwenda kufungua nione. Ghalfa nikamuona yupo upande wa pili anagonga. Sikumwambia chochote. Mlango ukafunguliwa akatoka mzungu. Sasa lugha pale ilikuwa changamoto Cannavaro akaishi kumjibu “sorry my friend” kila siku nikikutana na Cannavaro huwa namkumbushia hilo neno sorry my Friend” Abdi Kasim

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here