Home Kitaifa Chama anatisha kama kimbunga

Chama anatisha kama kimbunga

6096
0

Napenda kiujumla kuwapongeza wachezaji wa klabu ya Simba, kwa ushindi walioupata leo kwa kujituma kwa sababu ni moja michuano mikubwa Barani Afrika, napenda pia kuwaambia pia muendelee kujituma mutuwakilishe Tanzania, nyie ndo timu pekee mpo kwenye michuano hiyo. .
.
Clautious Chota Chama, moja viungo bora niliyowahi kuonana katika ligi kuu Tanzania Bara, huyu mchezaji ni kiungo mshambuliaji ni mzuri kwenye kutengeneza nafasi za mabao na hata kufunga ni wachache sana kupata viungo hawa huwa tunasema complete attacking midfielder, kwa maana ya kiungo mshambuliaji aliyekamilika kila kitu akiwa uwanjani.
.
.

Niliwahi kumsikia msemaji wa klabu ya Simba Haji S manara ,akisema Chama ana uwezo mkubwa sana uwanjani kama angepata nafasi alikuwa hata ana uwezo wa kuchezea klabu ya Arsenal, kwa umahili wake mkubwa uwanjani. .
.
Je unakubaliana na kauli msemaji wa klabu hiyo?me binafsi naweza tuyaheshimu mawazo yake Chama, huwa mara nyingi zaidi anacheza katikati juu ya Mkude, na Kotei, ndo maana tunamuona anakuwa uhuru zaidi ana uchezea mpira jinsi anavyotaka yeye. .
.
Katika mchezo wa leo dhidi ya Mbabane Swallow, alifunga mabao mawili ndani ya dakika nne kwa maana ya dakika 28 na 32 pia akapika bao la Meddie Kagere, me binafsi nasema Chota, amebarikiwa miguu ya dhahabu kwenye kuuchezea mpira na nafasi anayocheza inampa uhuru zaidi. .
.

Wakati Chama, amepika bao la Kagere, niliziona Camera zikimlenga msemaji wa Simba Manara akitabasamu kwa sababu anaamini ubora wa mchezaji huyo akiwa uwanjani timu inapita kitu Chama, uchezaji wake upole wake akiwa uwanjanj naweza kusema ni kama kiungo wa zamani wa klabu ya Barcelona, Andreas Iniesta. .
.

Iniesta,alikuwa mpole uwanjani anauwezo mkubwa kwa kukaa na mpira na hata kupiga chenga me nafikiri katika mchezo wa soka nidhamu na kujituma ndo mafanikio Chama, usibweteke usilewe sifa pambana zaidi ufike mbali una uwezo mkubwa sana. .
.
Katika michezo miwili dhidi ya Mbabane Swallow, umeonyeshwa kiwango kizuri sana hata mashabiki wa timu pinzani wanaelewa umuhimu wako ukiwa uwanjani.

Na Azziz Mtambo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here