Home Tetesi za Usajili Chelsea kumsaka mbadala wa Courtois, Rio aionya Man United

Chelsea kumsaka mbadala wa Courtois, Rio aionya Man United

11785
0

Klabu ya Manchester United, imegoma ofa kutoka kwa klabu ya Barcelona, kitita cha paundi million 45 na pamoja na wachezaji wawili ambao ni Andrei Gomes, na Yerry Mina, kama sehemu ya uhamisho wa kiungo wao Paul Pogba, kujiunga na Barcelona.

Klabu ya Chelsea, ipo tayari kutoa kiasi cha paundi millioni 89 kumnunua goli kipa wa klabu ya Athletico Madrid, Jan Oblak kama mbadala wa goli kipa Thibaus Courtois, ambaye hivi karibuni amekuwa akihusishwa kuondoka katika klabu ya Chelsea. Courtois, ameshindwa jana kurejea mazoezini katika klabu yake ya Chelsea, huku akitaka kuondoka Chelsea, na kujiunga na klabu ya Real Madrid. Chelsea wapo tayari kumsajili goli kipa wa Athletico Madrid, kabla dirisha la usajili halijafungwa.

Goli kipa wa klabu ya Manchester City, Joe Hart, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na klabu ya Burnley, na kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Burnley. Hart, mwenye umri wa miaka 31 ameshindwa kupata namba katika kikosi cha Manchester City, chini ya Pep Guardiola, anatarajiwa kukamilisha usajili huu ndani ya siku ya leo.

Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa England, Rio Ferdinand, amewambia klabu ya Manchester United, kumbakiza kiungo wao Paul Pogba, ambaye hivi karibuni amekuwa akihusishwa kuondoka klabu ya Manchester United, na kujiunga na klabu ya Barcelona. Ferdinand, amesema kuwa pia klabu ya Manchester United, imsajili beki wa kati wa klabu ya Tottenham, Toby Alderweiled, ambaye hivi karibuni amekuwa akihusishwa kuondoka katika klabu ya Tottenham. Alderweiled, amekubali kujiunga na klabu ya Manchester United, lakini Tottenham, wamesema kuwa mpaka wampate mbdala wake ndo watamuachia kuondoka. Ferdinand, amesema kuwa mpaka sasa klabu ya Manchester United, imesajili wachezaji wawili ambao kiungo wa klabu ya Shaktar Donetsk, Fred, na beki wa klabu ya Fc Porto, Diogo Dalot.

Takwimu za Joe Hart, akiwa na klabu ya Manchester City ndani ya miaka 12 aliyoitumikia.
Michezo 348
Makombe mawili ya ligi kuu England. Kombe la FA Mara moja.
Kombe la Efl mara mbili
Tuzo ya goli kipa bora mara nne.
# LEGEND

Tarehe 3 August, klabu ya Manchester United, ilifikia makubaliano na beki wa klabu ya Barcelona Yerry Mina.

Tarehe 4 August klabu ya Manchester United, ilifikia makubaliano na klabu ya Tottenham, kumsajili beki wa Kati Toby Alderweireild, ndani ya masaa 48.

Tarehe 5 August, klabu ya Manchester United, ilitangaza kuwa ipo tayari kutuma ofa kwa beki wa Leicester City, Harry Maguire.

Tarehe 6 August, klabu ya Manchester United, ilitangaza kuwa inataka kumsajili beki wa klabu ya Bayern Munich, Jerome Boateng.

Je unadhani beki gani atawafaa Manchester United.

Taarifa na Aziz Mtambo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here