Home Ligi BUNDESLIGA Chelsea kuvunja rekodi ya dunia, mjue mvunjaji

Chelsea kuvunja rekodi ya dunia, mjue mvunjaji

12237
0

Klabu ya soka ya Chelsea inakaribia kukamilisha kila kitu kumnasa mlinda lango wa Athletic Bilbao Kepa Arrizabalaga kwa ada ya £71m ambayo itavunja rekodi ya dunia kwa usajili wa walinda mlango(makipa).

Tayari Athletic Bilbao wamethibitisha kwamba Chelsea wanatoa kiasi hicho cha pesa kumnunua Kepa na hii inaweza kumfanga Thibaut Courtois kujiunga na Real Madrid.

Kepa Arrizabalaga ni nani?

Kepa Arrizabalaga Revuelta “Kepa” ni mzaliwa wa mjini Ondarrua nchini Hispania ambapo alizaliwa miaka 23 iliyopita (3/10/1994)

Kama hufahamu tu ni kwamba Kepa amekulia Bilbao na hao ndio waliomlea kwani kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2012 alikuwa akiichezea timu ya wadogo ya Bilbao.

2012 alipandishwa katika timu ya wakubwa ya Atletic Bilbao lakini mwaka 2015 alipelekwa katika klabu ya Valoid kwa mkopo kabla ya msimu uliopita kurudi tena Bilbao.

Kwa timu ya taifa Kepa amewahi kuichezea mechi moja tu, lakini amewahi kuwa kipa wa Hispania U-18 vile vile amewahi kuidakia timu ya Hispania U-19 katika michezo miwili.

Makipa 5 ghali dunia kabla ya Kepa.

1.Allison Becker (As Roma – Liverpoo) £65m.

2.Ederson (Benfica – Man City) £35m.

3.Gianluigi Buffon (Parma – Juventus) £32.6m.

4.Jordan Pickford (Sunderland – Everton) £30m.

5.Bernd Lano (Bayern Leverkusen – Arsenal) £22m.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here