Home Uncategorized Chelsea Vs Arsenal, inamweka tena Unai kwenye njia panda

Chelsea Vs Arsenal, inamweka tena Unai kwenye njia panda

10244
0
Zama mpya za Arsenal bado zinakumbana na changamoto nyingine kwenye suala la maamuzi ya yupi aanze na yupi akalie mkeka. Mchezo wa kwanza kwa Unai Emery kama kocha mpya dhidi ya Manchester City bado haujatoa muongozo sahihi kwa mwalimu huyu hasa baada ya kikosi kizima kuonekana kuelemewa.

Hata hivyo sio mwisho wa soka kwa mashabiki wa Arsenal bado wana matumaini na ujio wa mwalimu huyu. Kuna uwezekano kuwa kuwa falsafa tofauti zimeletwa na mhisipnia huyu licha ya kwamba mchezo wa kwanza haukua na matokeo yenye tija.

The Gunners wanatarajia kukutana na kigongo kingine Chelsea pale Stamford Bridge bila shaka mwalimu anapaswa kufanya mabadiliko makubwa kimfumo na upangaji wa wachezaji ili kuimarisha matumaini ya mashabiki. La sivyo atakuwa amejiwekea katika mazingira magumu sana hasa kipindi hiki ambpo uvumilivu ni gharama kuliko hata bei ya kununua bara zima.

Chini tutajaribua kuangazia ni kwa namna gani mwalimu anaweza kufanya katika upangaji wake wa kikosi hasa katika eneo la viungo.

 

 

Lucas Torreira

Arsenal hawakuridhika sana kumuona mchezaji huyu aliyenunuliwa tarkibani £26m akiingia kutokea benchi katika mchezo wao wa mwisho. Mchezo wa mwisho palionekana pana ugumu sana katika safu ya ulinzi ya kiungo hivyo kuna uwezekano mkubwa kabisa M’uruguay huyu ambaye anacheza mpira wa kazi na nguvu akaunganika kwenye safu ya viungo wa tatu ili kuleta ladha flani ya mpira wa nguvu kuweza kupambaana na N’golo Kante.

MSwiss huyu wa Arsenal kwenye mechi ya ufunguzi alipoteza mipira takribani 19 na kulaumiwa sana kwa kucheza chini ya kiwango. Xhaka alipangwa pamoja na Mattéo Guendouzil kwenye safu ya viungo wa wawili. Lakini inaonekana Gue alinonesha ukomavu wa hali ya juu licha ya ugeni wake tofauti kabisa na Xhaka ambaye tayari ni mzoefu. Alionekana kuwa mzigo kwenye kukaba na alikuwa mvivu wa kuhamisha timu. Ni mchezaji mzoefu sana kwa Arsenal hivyo sijui maamuzi ya Unai yatakuwa wapi lakini mchezo ujao itakuwa karata yake ya mwisho kupata imani ya Unai kama atafanya vibaya tena.

Mattéo Guendouzi: Mchezaji huyu wa zamani wa Lorient alionesha ukomavu wa hali ha juu. Alinonesha nidhamu kubwa sana pale timu ilipokuwa haina mpira na alionesha ujasiri mkubwa pale alipopokea mpira. Kijana huyu alimfanya Granit Xhaka kuonekana kama zuzu wa soka kwa kitendo cha kufanya majukumu yake na majukumu ya Xhaka kwa pamoja kama kuchezesha timu, kukaba na kushambuliaji. Kuna uwezeknao mkubwa Emery akamzawadia nafasi nyingine dhidi ya Chelsea

Aaron alinzishwa kwenye mechi dhidi ya Manchester City kama namba 10, ili kumchezesha Aubameyang. Mara kadhaa Ramsey amekuwa akitumika kama kiungo mchezeshaji au kiungo wa tatu katika safu ya viungo wa tatu akisaidia katika majukumu ya kukaba na kushambulia. Mchezo uliopita hakuwa na madhara sana na alishindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo baada ya Xhaka kushindwa kuunganisha timu vyema. Itategemea na majukumu atakayopewa mchezo ujao. Kama mwalimu atahitaji namba 10 inayotokea katikati bila shaka Ramsey ataanza lakini pia mwalimu anaweza kusukuma jukumu hilo kwa Ozil kutokea pembeni na Micky kulia hivyo Ramsey atakuwa kwenye kundi la kupigania namba dimba la kati akiwemo yeye,Elneny Torreira, Gue na Xhaka hivyo huenda kaanza benchi au Xhaka au yeyote.

Mesut Ozil: Mchezo uliopita ulimzidi sana Ozil kwenye suala la kuendana na kasi. Na ili kuifunga safu ya Man City unahitajika uwe mshapu sana. Ozil alitokea pembeni ili kumlisha Auba. Kuna wakati naamini kuwa Auba atafaa zaid kama akitokea pemben, Ozil acheze nyuma ya namba 9 kisha Micky upande wa wapili halafu namba 9 asimame Lacazette. Na mfumo utakaofaa hapo ni 4-2-3-1. Mchezo ujao sijajua mwalimu atatumia bado 4 3 3 au atabadili.

 Huyu Mmisri bado amekosa nafasi ya kudumu klabuni Arsenal. Yeye yupo yupo tu kama tipu iliyokwisha haribika. Anasubiria tu kusikia kuna pancha azibe. Kuna tetesi kwamba alikuwa mbioni kuuzwa au kutolewa kwa mkopo. Sijui na sioni nafasi yake sana labda kama itatokea suala la majeruhi. Mchezo unaokuja sijafaham kama Emery anaweza kumwamini labda kama atamtumia kama mchezaji wa ziada.

Mchezo wa mwisho huyu nae kama Ozil tu walikuwa wanakimbizana na kivuli cha ndege wakiwa na baiskeli. Walipewa jukumu ka kumlisha Auba lakini hawakufanikiwa. Mchezo ujao ni mgumu sana kwa mawinga wa pembeni wa Arsenal hasa ukiangalia wachezaji wa pembeni wa Chelsea ni wagumu no, Azpilicueta na Alonso. Kazi kwao

Sina imani kama ataanza lakini huyu nadhani ndiye mbadala wa Henrikh Mkhitaryan. Amesaini mkataba mpya bila shaka mwalimu amemwamini na atampa nafasi ya kutosha.

 Usisahau kwamba mchezo huu unaweza kuuangalia katika simu yako na ni ukiwa na application ya DSTV pekee, cha kufanya lipia king’amuzi chako uweze kuuona mtanange huu live.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here