Home Ligi EPL London Derby, Unai Emery kuifukuzia rekodi mbovu iliyodumu kwa miaka 26

London Derby, Unai Emery kuifukuzia rekodi mbovu iliyodumu kwa miaka 26

9980
0

Makocha wawili wapya katika EPL huku Maurizio Sarri kule Unai Emery hii leo wanakutana katika mchezo ambao utaoneshwa moja kwa moja kupitia DSTV channel za Super Sports.

Mchezo huu unaweza kuwa na presha kubwa kwa Unai Emery haswa ukiangalia ugumu na ukubwa wa Chelsea na wakati huo huo Arsenal walitoka kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Man City.

Chelsea wao wanaweza kuingia katika mchezo huu wakijiamini kutokana na kuwafunga Arsenal katika michezo mitano kati ya sita ambayo Arsenal walitembelea Stamford Bridge.

Pamoja na Alvaro Morata kutofanya vizuri lakini anaweza kuanza katika mchezo wa leo baada ya Sarri kusema anamuamini sana Mhispania huyo na ataendelea kumoa nafasi.

Kama Arsenal wakipoteza mchezo wa leo watakuwa wamepoteza michezo yao miwili ya kwanza ya ligi na hii haijawahi kutokea tangu msimu wa mwaka 1992/1993 na hivyo Emery atakuwa ameweka rekodi mbovu ambayo hata Wenger hajawahi kuiweka.

Kocha wa mwisho wa Arsenal kupoteza mechi mbili mfululizo(za michuano yote) alikuwa Steve Burtenshaw na ilikuwa mwaka 1986.

Lakini Arsenal wamefanikiwa kupata clean sheets mbili mfululizo Stamford Bridge na kama leo wakipata clean sheet nyingine itakuwa ya tatu mfululizo na hii itakuwa mara ya kwanza kwao kuwa na clean sheets 3 mfululizo katika uwanja wa Chelsea tangu 1924.

Rekodi ya Sarri katika uwanja wa nyumbani ndio inaogopesha zaidi kwa Arsenal, akiwa Napoli kocha huyo alipoteza mechi nne tu kati ya 57 katika uwanja wa nyumbani wa Napoli.

Kama Arsenal watashindwa kupata goli katika mechi ya leo baasi itakuwa mara ya kwanza kwao kushindwa kufunga goli katika mecho mbili mfululizo za ufunguzi wa ligi tangu 2012.

Kama Jorginho akifunga hii leo atakuwa mchezaji wa nne kufunga katika mechi mbili za kwanza za Chelsea baada ya Deco, Diego Costa na Adrian Mutu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here