Home Kimataifa Chelsea yamnyatia mfungaji bora EPL

Chelsea yamnyatia mfungaji bora EPL

6024
0

Chelsea kwa kipindi kirefu imekuwa na changamoto ya fowadi wa mwisho tokea Didier Drogba aondoke klabuni hapo. Washambuliaji wengi waliokuja Chelsea aidha walishuka viwango au wengine hawakudumu.

Baada ya kumkosa Lukaku msimu uliopita klabu ya Chelsea ilimgeukia Morata. Lakini Morata alishindwa kuhimili mikikimikiki ya EPL. Dirisha dogo wakamsajili Oliver Grioud.

Giroud na Morata msimu huu kwa ujumla wao wana mabao 6 tu. Kocha Mairizzio Sarri anajaribu kutafuta mbadala au mwarobaini wa tatizo la ushambuliaji.

Hivi majuzi Gianfranco Zola alisikika akimsifia sana mshambuliaji wa Bournemouth Collum Wilson kuwa mmoja kati ya washambuliaji bora.

Chelsea inasemekana inajiandaa kutoa dau nono la Paundi Milion 45 ili kunasa saini ya mfungaji huyo bora wa Bournemouth msimu huu akiwa na mabao 8.

Collum Wilson msimu uliopita alifunga magoli 8 katika michezo 28 akiwa na miaka 25. Msimu huu tayari amefunga magoli 8 katika michezo 15. Ufanisi wake mkubwa msimu huu uliweza kumshawishi kocha wa England Gareth Southgate kumuita katika kikosi cha timu ya taifa.

Collum alicheza mechi yake ya kwanza timu ya taifa katika mchezo maalumu wa kumuaga Wayne Rooney dhidi ya USA ambapo Wilson alifunga bao lake la kwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here