Home Kitaifa Chuji aikata maini Tanzania Prisons

Chuji aikata maini Tanzania Prisons

4330
0

Mechi nyingine kali siku ya leo ni Tanzania Prisons vs Coastal Union pale kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.

Kuna kila sababu ya kuishuhudia hii game, Prisons kwa namna yoyote ile watataka kushinda huu mchezo wakiwa nyumbani ili angalau wasogee nafasi za juu kutoka huko bondeni walipo sasa hivi.

Wajelajela wameshinda mechi moja tu kati ya 17 ambazo wameshacheza hadi sasa, wamepigwa mechi 8 na kutoka sare mara 8 kwa hiyo wana pointi 11 huku wakiwa nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi.

Endapo watashinda watafikisha pointi 14 na kukaa juu ya African Lyon yenye pointi 12 hadi sasa ikiwa nafasi ya 18.

CHUJI AIKATA MAINI PRISONS

Kiungo wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars ambaye kwa sasa yupo Coastal Union Athumani Idd ‘Chuji’ ameahidi kuongoza mapambano ya kutafuta ushindi dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa leo wa ligi kuu utakaochezwa uwanja wa Sokoine.

“Tumejiandaa kupambana kuhakikisha tunapata kilichotuleta, jitihada za mtu ndio zitamsaidia lakini upande wetu tutapata ushindi kutokana na maandalizi tuliyofanya”-Athumani Idd ‘Chuji’.

Yote haya yanaikuta Prisons ikiwa chini ya kocha bora wa msimu uliopita Mohamed Abdallah ‘Bares’ kumbuka pia Wajelajela walimaliza katika nafasi ya 4 msimu uliopita, kitu gani kinaisumbua Prisons? Unataka kujua? Usiache kutazama mbungi hii iwe kwa kwenda uwanjani au kupitia #AzamTV.

🏟game itakuwa uwanja wa Sokoine, Mbeya
🕓kuanzia saa 10:00 jioni
📺itakuwa LIVE kupitia Azam TV #AzamSports2 na #AzamTVApp

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here