Home Kimataifa Coulibaly amalizana na Al Ahly

Coulibaly amalizana na Al Ahly

4716
0

Salif Coulibaly raia wa Mali amevunja mkataba wake na klabu ya Al Ahly. Beki huyo akijiunga na Al ahly bure.

beki huyo aliichezea Al Ahly michezo 22. Coulibaly alifanikiwa kufunga magoli matatu na assist 2.

Coulibaly amekuwa na wakati mgumu klabuni hapo kwani katika michezo 7 ya mwisho alifanikiwa kucheza dakika 180 tu.

Coulibaly ameamua kuvunja mkataba wake na mashetani wekundu ili kupata nafasi katika timu yake ya taifa.

Kukosa namba katika kikosi cha Al ahly kukihatarisha nafasi yake katika kikosi cha Mali katika michuano ya mataifa huru ya Afrika.

Mpaka sasa hakuna taarifa zinazoelezea kuwa ataelekea klabu gani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here