Home Kimataifa Cr7 vs Ciro Imobille, kuagwa kwa Marchisio aisee mechi ya Juventus vs...

Cr7 vs Ciro Imobille, kuagwa kwa Marchisio aisee mechi ya Juventus vs Lazio sio ya kukosa

9670
0

Msimu huu kama unapenda soka ni lazima uwe na king’amuzi cha DSTV, kwani ukiwa umelipia DSTV halafu una app yao unaweza kuangalia mechi hizi kupitia tablet, simu ama laptop.

Usiku wa leo kwa mara ya pili Cristiano Ronaldo atakuwa uwanjani Serie A kujariby kutafuta goli lake la kwanza pale watakapoikabili Lazio.

Juventus wanaingia katika mechi hii na timu ambayo almanusra ibanwe mbavu na timu inayoonekana kibonde Serie A (Chievo) ambao wiki iliyopita walifungwa bao 3-2 kwa tabu sana na Juventus.

Lazio ni tofauti sana na Chievo kwani pamoja na kwamba wamepoteza mchezo wao wa kwanza kwa bao 2-1 dhidi ya Napoli lakini Lazio inabaki kuwa moja ya timu zinazogopeka Serie A.

Muitaliano Ciro Immobile atakuwepo kuongoza safu ya ushambuliaji ya Lazio na Immobile alifunga mabao 29 msimu uliopita na hii pekee inatishia safu ya ulinzi ya Juventus hii leo.

Battle kati ya Immobile na Cr7 ndio inaifanya mechi hii kuwa ya msisimko zaidi kwani hawa wote walikuwa vinara wa mabao msimu uliopita, Ronaldo akiibuka kinara Champions League na Immobile Serie A.

Jambo lingine la kusisimua japo chungu katika mchezo huu ni Claudio Marchisio, baada ya miaka 25 ndani ya klabu ya Juventus sasa mchezaji huyo anaondoka katika klabu hiyo.

Ameshaandika barua ya uchungu sana kuwaaga mashabiki wa Juventus lakini hii leo ataongea nao moja kwa moja na kuwaambia kwaheri jambo ambalo sio yeye tu bali hata mashabiki wa Juventus linawaumiza.

Tayari ameshawaandikia barua mbili lakini pia kwa kutumia video amewaaga ila vyombo vya habari nchini Italia vinasema Marchisio ameomba kuongea na mashabiki hao live leo uwanjani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here