Home Uncategorized Dakika 20 kabla ya Burnley vs United, mashabiki wa United kumfanyia jambo...

Dakika 20 kabla ya Burnley vs United, mashabiki wa United kumfanyia jambo hili Ed Woodward hii leo

11175
0

Kuwa kwenye timu kubwa wakati mwingine ni risk, na hivyo ndivyo unavyoweza kuamini kwani mashabiki wa vilabu vikubwa duniani kote hawaamini kama wao wanaweza kufungwa.

Michezo mitatu tu ya mwanzo ya msimu wa 2018/2019 umetosha kwa mashabiki wa United kuanza chokochoko kwa kocha wao Jose Mourinho pamoja na mkurugenzi wao Woodward.

Kuelekea katika mechi yao ya leo vs Burnley kuna kikundi cha mashabiki wanaojiita A Voice from Terrace wamejiandaa kurusha bango kubwa la kumtaka Ed Woodward aondoke na awaachie timu yao.

Bango hilo limeandikwa “Ed Woodward ni specialist wa kushindwa” litaruka hewani dakika 20 kabla ya mchezo kuanza na DSTV watakuonesha tukio hilo kutokea uwanja wa Turf Moor.

Na hii ni sababu ambayo itanifanya hiu leo mapemaa nitaangalia Super Sports 3 kuangalia jambo hili ambalo mara ya mwisho nililiona Arsene Wenger akifanyiwa na mashabiki wa Arsenal.

Turf Moor ni sehemu ambayo sio ngumu kwa United kwani wameshashinda hapa mara 8 wakatoka suluhu mara 8 na mara moja tu waliyopoteza hapa katika mechi 17 zilizopita ni mwaka 2009 walipofungwa bao 1-0.

Na cha kujiamini zaidi kuhusu United ni kwamba katika mechi 10 walizocheza katika uwanja huu, kulikuwa na clean sheets 9 kwao na hiyo 2009 ndio ambayo waliruhusu nyavu yao kuguswa na Burneley kwenye uwanja huu.

Kocha wa Burnley Sean Dyche ni kibonde kabisa wa Mourinho na katika mechi 6 walizokutana hajawahi kumfunga Mou, akiambulia vipigo 3 na suluhu 3.

Tayari United wameshapoteza michezo yao miwili katika mechi 3 za mwanzo za ligi ila kama watafungwa hii leo itakuwa vipigo vitatu katika mechi nne, mara ya mwisho United anapigwa mechi 3 katika 4 za mwanzo ilikuwa ni msimu wao wa 1986/1987.

Lakini mara ya mwisho pia kwa United kupewa vipigo viwili mfululizo ugenini katika ligi ilikuwa 1973, nini kinawatokea hii leo? Wataanza upya au ndio mwisho wa Mou na Woodward? Angalia DSTV.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here