Home Kitaifa De bruyne nje miezi miwili, Sasii pilato atakayewahukumu Simba na Mtibwa

De bruyne nje miezi miwili, Sasii pilato atakayewahukumu Simba na Mtibwa

8794
0

Kwa mujibu wa Independent na L’equipe wameripoti kuwa Liverpool wapo kwenye nafasi nzuri ya kumsainisha mkataba wa awali (pre contract) kiungo wa PSG Adrien Rabiot ifikapo Januari. Kiungo huyo ambae ni shabiki wa kutupwa wa Liverpool ameonesha nia ya kutaka kutua Liverpool licha ya Barcelona kumtaka pia.

Kiungo wa klabu ya Manchester City, Kelvin De Bryune, amepata majeraha ya goti leo wakati anafanya mazoezi na timu yake kujiandaa na mchezo wa ligi kuu week end ijayo. De Bryune, atakaa nje miezi miwili kuuguza majeraha yake ya goti.

Kevin De Bruyne atazikosa mechi zifuatazo

Huddersfield Town (h)
Wolves (a)
Newcastle Utd (h)
Fulham (h)
Cardiff City (a)
Brighton (h)
Liverpool (a)
Burnley (h)

Mchezaji wa klabu ya Chelsea, na timu ya taifa Nigeria, anaemia kustafuu kuitumikia timu ya taifa Nigeria. Moses, ameichezea taifa hilo michezo 37 na kufunga mabao 12.

Waamuzi wa mchezo wa ngao ya hisani kati ya Simba, dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa Jumamosi, Agosti 18 Mwaka huu kwenye dimba la CCM Kirumba, jijini Mwanza, wamewekwa hadharani.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) , waamuzi hao ni kama wafuatavyo mwamuzi wa kati ni Elly Sasii, kutoka Dar es salaam, waamuzi wasaidizi ni Fernand Chacha, kutoka Mwanza, na Helen Mduma, kutoka Dar es salaam. Waamuzi wa akiba ni Jonesia Rukya, kutoka Kagera, na mwangalizi wa waamuzi ni Alfred Rwiza, kutoka Mwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here