Winga wa Barcelona na timu ya taifa ya Uafaransa Ousmane Dembele jana kwenye mchezo dhidi ya Leganes aliumia kifundo cha mguu
Mchezo huo uliisha Kwa Barcelona kushinda goli 3 kwa 1. Magoli ya Suarez Dembele na Messi.
Dembele vs Leganes
66 Dakika
15 alikokotoa mpira
Kocha mkuu wa klabu hiyo Ernesto Valverde alithibitisha hayo.
“Ni kweli ameumia kifundo cha mguu wa kushoto. Nina imani ni jeraha dogo la leo atafanyiwa vipimo. Sidhani kama atakaa nje muda mrefu. Nadhani tuwe na subira tusikie madaktari watasemaje”
“Dembele amekuwa mchezaji wa muhimu sana kwetu. Kwa sasa ni tegemeo kubwa kwa klabu yetu. Namtakia kheri na augue pole. Najua atarudi muda sio mrefu” Sergio Busquet
Dembele Barca:
51 Mechi
17 Magoli
14 assists