Home Kitaifa Dilunga: Simba ni sehemu sahihi na jina lako ni baraka

Dilunga: Simba ni sehemu sahihi na jina lako ni baraka

13852
0

Baraka zinapokuja hakuna wa kuzuia. Ni Mungu tu ndiye atakaeamua. Hassan Dilunga ni mchezaji mwenye bahati kubwa sana kwa sasa. Amekuwa na msimu mzuri na Mtibwa Sugar na hatimaye kwa sasa yupo Uturuki. Anatarajiwa kupanda ndege safari kadhaa msimuu ujao.

Novemba 14 mwaka 2013 klabu ya Yanga ilifanikiwa kumpata Hassan Dilunga kutoka timu ya Ruvu Shooting. Miaka 4 baadae Mtibwa Sugar ilikamilisha usajili wa kiungo Hassan Dilunga kutoka JKT Ruvu mnamo julai 24 mwaka 2017.

Miezi 11 baadae tarehe 13 mei 2018 mnamo dakika ya 82 ikirindima ikiwa ni siku ya kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa Dilunga alifanikiwa kuifunga Yanga bao pekee. Sina maana kwamba ilikuwa zawadi yake kwangu siku ya kuzaliwa la hasha maana mashabiki wa Yanga wanaweza kudhania naishabikia Simba. Sishabikii yeyote hayo.

Uzuri wa Dilunga anajiamini mno. Na anajikubali hasa kile anachokifanya uwanjani. Hicho ndicho kitu nilichokiona kwake. Mara ya mwisho aliniambia Azam sio timu kubwa kama Mtibwa hivyo hawatatusumbua. Ni kweli. Walifanikiwa na wakatwaa ubingwa wa FA.

Rafiki yangu Dilunga utakaporudi ligi kuu utakumbana na mengi sana. Najua wapo wanaowaza nafasi yako ndani ya Simba. Hilo wala lisikutishe. Kuna mtu anaitwa Mo Salah. Alikwenda Liverpool iliyokuwa na Mane, Coutinho, Firmino na Lalana. Lakini alichokifanya kila mtu alishangaa.

Pia yupo mdogo wako anaitwa Rashford. Alitokea zake shule ya msingi huko, huenda alikuwa anawaza kivipi atapata nafasi ya mkopo hata Derby Country huko, ila yupo Mungu, aliyemtoa chini ya kivuli cha akina Rooney, Depay na Chicharito na akafanya makubwa. Pia usisahau kuhusu Assensio na Vasquez.

Dilunga unatembelea jina la mchezaji mkubwa kuwahi kutokea kwenye historia ya Yanga na Simba. Wala usiogopeshwe sana na maneno ya watu kwamba uliwahi kucheza Yanga na hukuondoka kwa mema. Hata Marehemu Maulid Dilunga alicheza Simba na Yanga tena wakati anaondoka Simba aliondoka kipindi cha mgogoro. Hakuwa na ufanisi mzuri sana Simba mpaka Simba iligawangika mara mbili na kutokea Nyota Nyekundu. Changamoto za maisha ni sehemu tu ya kipimo cha ufanisi wako. Uzuri wa uwanja wetu mashabiki wapo mbali sana na uwanja hivyo hata ukitukanwa huwezi kuyasikia.

Dilunga pambana uweze kusafisha nyota hii ya mzee Maulid Dilunga iliyofifia baada ya kifo chake 2008.

Kombe la FA pekee halitoshi ikiwa wajina wako aliwahi kufuatilia mpaka na Klabu ya West Bromwich ikimtaka awafanyie kazi. Mzee Dilunga alicheza timu ya taifa kwa miaka 10 hili ni deni kubwa sana kwako pia. Huyu Mzee Dilunga ndiye aliyekuwa kiboko ya Waghana alipowafunga bao lilillawatoa mashindanoni mwaka 1973 kule Lagos. Una deni kubwa bro la jina hili la Dilunga. Mtibwa haina mashabiki wengi wala Simba haina mashabiki wengi kuliko mashabiki wa taifa stars. Tunakuhitaji tukuone Star na ufanye makubwa

Mzee Dilunga ana mafanikio makubwa sana. Aliwahi kuitwa kwenye kombaini ya Afrika baada ya kufanya vyema na timu ya taifa. Tanzania ilisuluhu na Nigeria wakaifunga Ghana na Togo, na mabao yote ya stars yalifungwa na Dilunga. Mchezo uliofuata ulipigwa uga wa Surulere, Lagos, wakadroo na Nigeria, kabla ya kutoshana nguvu na 1-1 Misri.

Hata hivyo Stars ilitupwa nje kwa mabao mawili 2-1 dhidi ya waarabu wa Algeria. Dilunga alipachika mabao 4 kati ya 5 yaliyofungwa na stars ndio maana aliweza kuchaguliwa katika kikosi cha kombaini ya Afrika, ambacho kilizuru mataifa mbalimbali ya Amerika na Ulaya, kucheza mechi za kirafiki. Walifanikiwa kwenda Mexico, Guatemala, Uruguay, Peru, Hungary na Bulgaria.

Rekodi nzuri ya Mzee Dilunga sio kitu ndugu yangu Hassan. Kuna mtu aliitwa Ronaldo De lima. Alikuwa na jina kubwa duniani miaka 2002. Alilitawala soka lote la ulaya na amerika. Alikuwa fowadi bora kwa wakati huo. Miaka kadhaa baadae alitokea bwana mdogo kutoka Madeira wakuitwa Cristiano nae pia ni Ronaldo. Wabrazil wengi walimdhihaki kwamba Ronaldo ni mmoja tu duniani. Nadhani tulipokutana mara ya mwisho mimi na wewe tulimzungumzia Ronaldo. Uliniambia unampenda Ronaldo kwa sababu anajiutma. Usiogope majina utakayokutana nayo Simba. Wala usiogope jina kubwa la Dilunga ila ogopa kufeli. Jina kubwa ni baraka. Tembelea nyota hiyo. Dilunga Simba ni sehemu sahihi kama ulivyoamua. Wala usiogope majina utakayokutana nayo. Chuma hunolewa na joto kali. Pambana sana.

Huenda una kipaji, lakini Canavaro neno la mwisho aliniambia kipaji sio tija kama mtu hajitambui. Wewe tayari upo kwenye histotia ya kichwa changu, wewe ni mchezaji mkubwa sana. Kitendo cha kufanikiwa kucheza vilabu vikongwe vitatu (Mtibwa, Simba na Yanga wewe ni bora) Una uwezo ulichobakiza ni deni letu tu, kutuonesha ulicho nacho. Kila la kheria Hassan Dilunga.

Hapa upo kwenye website ya Shaffih Dauda, pia tuna ukurasa wa Instagram na facebook kwa jina hilo hilo, huko utakutana na taarifa nyingi na za uhakika. Usiache kutembelea YouTube channel yetu ya Dauda Tv. Tena nikukumbushe Abdi Banda kaoa. Nenda ujionee

Mimi naitwa Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here