Home Kitaifa Dkt Magufuli ameleta ndege mpya, na Simba imeleta ushindi mnono

Dkt Magufuli ameleta ndege mpya, na Simba imeleta ushindi mnono

4419
0

Kama ulikua hujui leo Taifa la Tanzania limeandika historia nyengine kwa kuweza kununua ndege Mpya aina ya A 220-300 . Ndege hii imepokelewa na Raisi wa jamuhuri wa muungano Dkt .John pombe Magufuli .

Wakati Simba wanaingia uwanjani saa 10 kamili uwanja wataifa (kwa mchina) Raisi Magufuli ndo alikua anamalizia hotuba yake kwa nchii na ikawa inasubiliwa ndege. Wakati wakusubirii ndegee Nkana walipata goli dakika ya 17′ kupitia kwa mshambuliaji wao walter Bwalya.

NDEGE aina ya Airbus ilitinga Katika Anga la Dar es Saalam na kushangiliwa na wananchi waliojitokeza kuipokea ila hapo hapo ndipo kiungo fundi Johnas MKUDE alifungaaa Goli la mbalii na kuisawazishia simba na kuifanya simba kwenda moja moja na nkana.

Ndege ya Magufuli imegusa ardhi ya Tanzania wakatii tayari Simba Wapo nguvu sawa na Nkana .dakika 45 simba ilijipatia Goli la pili kupitia kwa Kagere nakuifanya Simba kua mbele ya nkana kwa magoli mbili moja na kuenda mapumziko.


PATA KIFURUSHI

Regional breakdown

CAFCL group stage

Kaskazini mwa Africa – timu 7

Kusini mwa Africa – timu 3

Africa Magharibi – timu 3

Africa ya kati – timu 2

Africa Mashariki – 1


Dakika ya 89 simba iliandika goli la 3 kupitia kwa Fundi wao CHAMA Kutoka kwa pasi sukari ya Dilunga. Bao ambalo limewapeleka simba hatua ya makundi hii ni baada ya kupita muda mrefu tangu 2003.

Wakatii ndege inaonekana kwenye anga la Daresalam na mkude akairudishia uzima simba na wakati Nchi inasherekea kuja kwa nDege na mashabiki wa simba wanasherekea kuvuka hatua ya makundi.

Nitoe pongezi kwa Raisi na wananchi wote ila kwa ndugu zangu simba hongereni na kama taifa tunasema Asanteni kwa kututoa kimaso maso… hii ilikua ni siku ya historia kwa nchii.. Hii ndege ina kituuuu na simba…(jokes)

Ujumbe kutoka kwa Edgar Edson

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here