Home Kimataifa Drama za Perez zitawaponza Chelsea

Drama za Perez zitawaponza Chelsea

6272
0

Tumesikia Isco anauzwa. Lakini tujiulize kwani Isco Madrid kachoka? Kwani Madrid hakuna nafasi ya Isco? Si ndio Isco yule yule Perez akichukua uamuzi mgumu kumruhusu Di Maria kuondoka ili ampishe Isco kutoka Malaga?

Kila mtu anajua Isco aliletwa kwa msaada wa Zidane. Huenda Perez hakuwa na upendo kwa Isco kiasi cha kumfukuza Di Maria bali alisikiliza ushauri wa Zidane.

Isco leo yupo benchi, Perez anaona, nani wa kumtetea Isco zaidi ya Zidane? Hakuna. Kwanini hachezi? Hizi ni mbinu za Perez tu. Sura halisi ya Perez inaonekana. Perez uvumilivu umemshinda. Anamtumia kigezo cha kumnyima amani Isco ili akamilishe mipango yake.

Zidane alisema aliondoka Madrid kwa sababu Perez alitaka kuingilia kati sakata la usajili. Perez alihitaji kumwaga mihela kuleta mastaa na Zidane aliwaamini vijana wake. Alijua mastaa wakijaa akina Assensio na Isco hawatapata nafasi. Ni kazi sana kuwavumilia mastaa wa kizazi hiki.

Si unakumbuka watu kama Tedd Sherringham na Ole Gunnar walitokea benchi United lakini leo hii ukimweka Martial au Pogba benchi kazi huna? Zidane hakutaka kupangiwa chochote. Perez alitaka kuendelea kuitawala Madrid kwa kufanya usajili wa mastaa ambacho kido kigezo ambacho kitamfanya awe raisi wa kudumu Madrid.

Leo tunasikia Isco anasakamwa na benchi. Benchi limemkaa kwelikweli. Hana mtetezi. Man City wamekwenda kuulizia bei wameambiwa walete Paundi 100 Chelsea nao wamekwenda wameambiwa leteni 70! Hivi umeelewa utofauti wa Chelsea na City? Kama hujajua basi Perez anataka kutegua kitendaliwi ambacho Zidane alikataa.

Yaani Perez yupo tayari kumuuza Isco 70 kwa Chelsea ili kuwaweka kwenye mtego wa kumpata Hazard. Isco ametumika kama chambo ya Hazard na si vinginevyo. Perez alimhitaji sana Hazard ndio maana hakuona tabu kumruhusu Zidane aende ili ampishe kufanya usajili anavyojisikia.

Perez amekubali kuwapunguzia Chelsea Paundi milioni 30 tofauti na Man City ili tu apate nafasi ya kumnasa Hazard. Usishangae kusikia Real wametoa 30 pamoja na Isco ili wampate Hazard.

Isco anaifaa sana Chelsea kwa sababu hawana kiungo mbunifu anayeeleweka kwa sasa. Fabregas haaminiki tena, Kante sio mbunifu na Jorginho pia sio mbunifu kivile. Kovacic sio mchezaji wao na wanafahamu fika nafasi hiyo ni ndio link muhimu zaidi hasa katika mfumo wa Sarri ball.

Chelsea huu ni mtihani kwao, aidha watoe 45 wampate Collum Wilson watulie, au wakubali kumnasa Isco na kuweka hali ya hatari kumzuia Hazard. Ujanja wa Perez kuwabembeleza Chelsea kwa ajili ya Hazard ulianza tokea pale alipowapa Kovacic kwa mkopo


PATA KIFURUSHI:

Thorgan Hazard: Bundesliga

👤 16 Michezo
⚽️ 9 Magoli
🅰️ 7. assists

Eden Hazard: Ligi kuu

👤 16 Michezo
⚽️ 8. Magoli
🅰️ 9. assists

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here