Home UEFA Champions League Droo ya klabu bingwa Ulaya kutia nanga leo! Atletico yaipiku Man United,...

Droo ya klabu bingwa Ulaya kutia nanga leo! Atletico yaipiku Man United, Liverpool yatupwa kwa vibonde

14998
0

KLABU BINGWA BARANI IMERUDI TENA


Leo tutashuhudia droo ya hatua ya makundi itakayofanyika kuanzia saa 11 jioni.
Real Madrid
Real Madrid ndio Mabingwa watetezi wa kombe hilo

Vilabu vinne vya England vitashiriki hatua ya makundi ya UEFA msimu huu mpya.

Manchester City itakuwepo kwenye kibubu cha kwanza, Manchester United na Tottenham Hotspur zimewekwa kibubu za pili, wakati washindi wa pili wa kombe hili Liverpool wapo kwenye kibubu cha tatu.

Droo hii itafanyika Grimaldi Forum nchini Monaco 17:00 kwa saa sa England ambapo huku kwetu itakuwa saa 1 kamili.

Mabingwa watetezi Real Madrid kama kawaida watakuwa kibubu cha kwanza pamoja wenzao Barcelona, Bayern Munich, Juventus, PSG na Lokomotiv Moscow, bila kuwasahau Atletico Madrid. Timu za Hispania tatu zimeingia kibubu cha kwanza.

Droo itafanyika vipi?

Bingwa wa Champions League na yule Europa League wao wanapata nafasi ya moja kwa moja kuingia kwenye kibubu cha kwanza. Pia mabingwa wa wa ligi kubwa 6 nao watapata nafasi hiyo.

Orodha ya ligi 6 bora duniani.

No Ligi Alama Timu
1 Spain Spain 104.998 4
2 Germany Germany 79.498
3 England England 75.962
4 Italy Italy 73.332
5 France France 56.665 3
6 Russia Russia 50.532

 

Kwanini Hispania Zimepita tatu kwenye kibubu cha kwanza?

Real Madrid Bingwa wa Uefa

Atletico Bingwa wa Europa

Barcelona Bingwa wa La liga.


Pot 1

 • Real Madrid
 • Atletico Madrid
 • Barcelona
 • Bayern Munich
 • Manchester City
 • Juventus
 • Paris Saint-Germain
 • Lokomotiv Moscow

Vibubu vingine vinaamuliwa kutokana na namna klabu ilivyofanya vizuri katika michuano ya Ulaya kwa muda wa miaka mitano.


Pot 2

 • Borussia Dortmund (89.000)
 • Porto (86.000)
 • Manchester United (82.000)
 • Shakhtar Donetsk (81.000)
 • Benfica (80.000)
 • Napoli (78.000)
 • Tottenham (67.000)
 • Roma (64.000)

Pot 3

 • Liverpool(62.000)
 • Schalke (62.000)
 • Lyon (59.500)
 • Monaco (57.000)
 • Ajax (53.500)
 • CSKA Moscow (45.000)
 • Valencia (36.000)
 • PSV Eindhoven (36.000)

Liverpool walitarajia labda kama Benfica angetolewa na Greek club PAOK ilo wao wapate nafasi ya kuingia kibubu cha pili lakino klabu hiyo ya Ureno ikpaya ishindi wa jumla ya mabao 5-2. Liverpool atakuwa kwenye kundi ambalo lazima litajumisha Mabingwa hivyo anaweza akajikuta kwenye kundi gumu

Pot 4

 • Viktoria Plzen (33.000)
 • Club Brugge (29.500)
 • Galatasaray (29.500)
 • Young Boys (20.500)
 • Inter Milan (16.000)
 • Hoffenheim (14.285)
 • Red Star Belgrade (10.750)
 • AEK Athens (10.000)

Hatua ya makundi itaanza lini?

Mechi za Champions League group zitaanza kutimua vumbi 18 na 19 Septemba mechi takribani 6 zitachezwa kabla ya raundi nyingine kuendelea 11 au 12 December.

Mtoano ni mwezi wa pili na fainali itapigwa uwanja wa  Atletico Madrid’s Wanda Metropolitano tarehe 1 June, 2019.


Ila Chelsea na Arsenal nadhani mtatupa ushirikiano mzuri kufuatilia michuano hii msitususie bado nyie ni ndugu zetu tehe tehe.


 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here