Home Kimataifa Eddie Howe ni bonge moja la kocha

Eddie Howe ni bonge moja la kocha

3770
0

Huyu ndie Kocha mkuu wa AFC Bournemouth kwa sasa na ameishi katika soka kwa kucheza pia kama Beki wa kati. Safari yake ya soka ilianzia katika Klabu hiyo hiyo ya AFC Bournemouth. Alizaliwa 29/Nov/1977

Alifanikiwa kucheza michezo 313 tuu akiwa na klabu hiyo ya Bournemouth lakini pia aliweza kucheza vilabu viwili tofauti ambavyo hakucheza kwa mafanikio makubwa.

Mwaka 1994-2002 alichezea klabu yake ya AFC Bournemouth na kuifungia magoli 10. Kisha akauzwa kwenda timu PORTSMOUTH mwaka 2002-2004 ambapo hakucheza sana alifanikiwa kuchezea timu hiyo mechi 2 tuu.

Mwaka 2004 timu yake Ya PORSMOUTH wakaamua kumtoa kwa mkopo kwenda SWINDON TOWN kwa mkopo ambako pia hakutumikia timu hiyo. Ndipo mwaka huo huo 2004 AFC Bournemouth wakamrejesha.

2004-2007 alifanikiwa kuchezea timu hiyo michezo 53 na kufanikiwa kufunga Goli moja tu. Alistaafu baada ya kua na majeraha ya Goti .

Alipewa mkataba wake wa kwanza na klabu yake ya AFC Bournemoth kama Kocha mkuu wa klabu hiyo akiwa na umri mdogo wa miaka 31 na hii ni baada tuu ya kustaafu kucheza soka. Mkataba wake wa kwanza ulikua 31/12/2008.

Aliiongoza timu hiyo na kuinusuru isishuke daraja katika ligi ya Championship. Aliweza kuiongoza AFC Bournemoth kama Kocha mkuu mpaka 15/1/2011 huku akiwa amecheza mechi 99 tuu.

Ndipo klabu ya Burnley ilipo msajili msimu wa 2011-2012 ambapo hakukaa kwa muda mrefu na kufanikiwa kucheza mechi 86 akiwa na timu hiyo na kisha kuamua kurejea AFC Bournemoth.

Alipewa timu ya Bournemouth kwanzia 14/9/2012 hapo ndipo mafanikio yake na timu hiyo yalipoanza baada ya kupigana na timu hiyo na mwaka 2015/2016 huu ndo msimu ambao rasmi kijana mdogo kabisaa aliweza kuweka rekodi ya kwa mara ya kwanza kuipandisha timu hiyo ya AFC Bournemouth ligi kuu nchini England (EpL)

Amekua Ligi kuu mpka sasa ni misimu mitatu tofauti na ameweza kujenga timu ambayo inaushindani sana katika ligi. Msimu huu wakati unaanza timu yake ilikua ni kizuizi sana kwa timu nyingi. Kwa sasa anashika Nafasi ya 12 katika ligi na mwezi wa 11 alipewa tuzo ya kocha Bora wa mwezi na chama cha soka FA.

Eddie Howe amefanikiwa sana katika maisha yake ya soka akiwa na Bournemouth hata enzi za uchezaji wake ametumikia klabu hiyo jumla ya michezo 313 ila katika timu zengine ameweza kucheza michezo miwili (2) tuu. Na ameweka rekodi ya kua Kocha mdogo zaidi katika ligi kuu nchini England akiwa na miaka 41 tuu.

Huyo ndo Howe kipenzi cha ATHLETIC FOOTBALL CLUB BOURNEMOUTH .

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here