Home Kitaifa Edigar Kibwana na Geof Lea wamvulia kofia Makambo

Edigar Kibwana na Geof Lea wamvulia kofia Makambo

16724
0

Heritier Makambo, Heritier Makambo hili ndilo jina lililokamata sana vichwa vya habari baada ya Yanga kuichapa Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1.

Makambo amekuja Yanga akitokea kwao Congo lakini wengi hawakuwa wanamuamini kutoka na usajili wake kutokuwa na mbwembwe kama ya sajili nyingine Tanzania.

Lakini Makambo amejijengea heshima kubwa kutokana na kufanya kile ambacho Wanayanga wengi walikimiss(kupasia nyavu), wachambuzi wa soka nchini Edgar Kibwana na Geoff Lea wana naoni yao kuhusu Makambo.

Edgar Kibwana

Makambo anaendelea kuongeza kitu kwenye klabu ya Yanga, wakati wa pre-season inawezekana watu wengi hawakumfaidi kama wanavyomuona sasa hivi.

Ni mchezaji ambaye ana kilakitu, ukiacha urefu wake ambao anajua vizuri kuutumia, alifunga magoli mawili dhidi ya Mtibwa ikiwemo ambalo lilikataliwa ambalo lilikuwa ni la offside lakini ukiangalia mipira mingi ya juu anafanikiwa kuicheza.

Ana kasi ana footwork nzuri akiwa na mpira hata asipokuwa na mpira anavyocheza kwenye eneo la hatari ni ngumu sana kumkaba hasa kwa beki ambaye hayupo makini.

Geoff Lea

Kuna washambuliaji ambao maeneo mengine huwa hawana kasi lakini wanapokuwa kwenye eneo la hatari wanakuwa na kasi ‘short sprint’ Makambo ana hicho kitu lakini pia ana nguvu za kummudu beki.

Mabeki wengi wa kitanzania wanachangamoto ya kuwa na miili midogo kwa hiyo Makambo atakuwa na faida ya urefu kuliko mabeki wengi.

Ni mchezaji mzuri Yanga wamemsajili, mimi sikuhitaji kumuona katika mechi nyingi baada ya kumwona kwenye mchezo dhidi ya USM Alger.

Labda kama alipania sana kwenye mechi ile lakini mimi palepale nilikubali kwamba Makambo ni mchezaji, ameshafunga katika mechi mbili mfululizo nafikiri ana mengi ya kuwafurahisha mashabiki wa Yanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here