Home Ligi EPL Epl hii hapa na Dstv wanaileta Man United vs Leicester City viganjani...

Epl hii hapa na Dstv wanaileta Man United vs Leicester City viganjani mwetu hii leo

10395
0

Kwa miezi mitatu na zaidi tumesubiria ligi kuu nchini Uingereza Epl na hatimaye hii leo msimu mpya wa 2018/2019 unatarajia kuanza kwa klabu ya Manchester United kufungua dimba dhidi ya Leicester City.

DSTV ndio sehemu pekee ambayo hii leo utaangalia mtanange huu moja kwa moja kupitia channel zao za Super Sports pale ifikapo saaa nne usiku, na jambo la kuvutia ni kwamba huangalii kwenye Tv tu.

Unaweza kudownload app ya DSTV kwenye simu yako au Tablet na ukweza kuangalia mtanange huu na mechi zote zijazo popote pale ulipo ukiwa na app hii, sio lazima uwepo kwenyw Tv kama ilivyokuwa zamani.

Leicester City sio warahisi lakini pia watu wanasubiri kuona namna ambavyo Manchester United wanaweza kufanya msimu huu wakiwa hawajasajili kama ambavyo wengi wamezoea.

United wanakwenda katika mchezo wa leo na matumaini ya kupata walau alama kutokana na rekodi ya kocha wao, Jose Mourinho hajawahi kupoteza katiak mechi ya ufunguzi Epl, ameshinda 8 na suluhu 1.

Katika misimu 17 iliyopita ya EPL ni Swansea pekee ndio ambao walifanikiwa kuifunga Manchester United katika mchezo wa ufunguzi wa EPL na hiyo ilikuwa mwaka 2014.

Lakini wakati United wakienda katika mchezo wa leo huku wakijiamini, Leicester wenyewe hali ni tofauti kwani katika mechi zao 9 za ufunguzi wa ligi wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu 2015 vs Sunderland.

United wameshawafunga Leicester katika mechi 13 za ligi lakini katika mechi ambayo United hawawezi isahau dhidi ya Leicester ni kipigo cha mabao 5-3 walichokipewa mwaka 2014.

Katika mechi 44 za ligi kuu ambazo Leicester City wamecheza dhidi ya Manchester United wamepata ushindi mara tatu tu, huku mwaka 1998 ikiwa mara yao ya mwisho kuifunga United Ot.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here