Home Kimataifa EPL mwaka unaisha kama hivi yaani

EPL mwaka unaisha kama hivi yaani

4810
0

Ligi pendwa Duniani ligi ambayoo inafuatiliwa na watu wengi sana duniani. Ligi ambayo wachezaji wengi wakicheza hua ni kama Dream comes True.

Mwaka 2018 unaisha ila pia ulikuwa una mwanzo na hua hii ligi kabla haijafika huwa bingwa anapatikana wa 2017/2018 na aliepewa ubingwa mwaka huu ni Man City ndo alitwaa ubingwa chini ya kocha wao Pep Gurdiola ikiwa ndo mara yake ya kwanza tangu ajiunge na miamba hiyo ya waarabu.

Hii ligi inaongoza kukusanya makocha wengi wenye CV’s kubwa sana Ulimwenguni hii ndo ligi inayo walipa pesa nyingi ukitoa ile ya mabeberu wa soka China. Ndani ya huu mwaka tumeona baadhi ya matukio makubwa ambayo yameingia kwenye kitabu cha historia za soka Duniani.

MAKOCHA kufukuzwa

Wakati ligi hii inakaribia kuanza yani 2018/2019 kulikua na kocha wa chealsea ambae hawezi kusahaulika kutokana na mbwembwe na mikogo yake akiwa kwenye eneo lake la kazi (Touch line) . Huyu ndo kocha ambae aliendana na mashabiki wa timu yake. Mashabiki walimpenda sana lakini viburi vyake kuvimbishiana misuli na mchezaji wake wa zamani Costa ndiko kuliko Mng’oa bwana huyu katika timu hiyo.wakati chelsea inamleta Morata yeye Aliamini hKuna striker kma morata duniani na kuanza kumletea nyodo costa ila alichouziwa na Madrid ni sawa na kununua na Mbuzi kwenye Gunia!..

KUna mtu mwenye kujiaminii , mtuu alieishi kwenye rekodi zake, mtu ambae waandishii waliona kufanya nae interview ni sawa na Necta nae si mwengine ni Mourinho kocha wa Manchester United. Huyu katika msimu wake wa kwanza alifanikiwa kushinda mataji matatu kwa mwaka likiwepo lile ambalo ibrahimović na sifa zake zote alishindwa kulitwaa nalo ni Europa.

Bwana Mou alitimuliwa na Man United mwishoni kabisa mwa mwaka huu baada ya kuitumikia club hiyo kwa miaka mitatu. Aliishi sana kirekodi bila kujua mashabiki wengi zile walikua gawazitaki walitaka nao waandike zao. Falsafa zake zilikuja kuumbuliwa ndani ya mchezo mmoja wa Ole gunnar solskjaer kua zilikua za kujilinda sana na kunyima uhuru wachezaji mpira ambao mashabiki wa united hawakuutaka kabisa.

Klopp huyu ndo mjerumani pekee alieingia Fainali saba kubwaa ila aliishia kuingia uwanjani na kuwapongeza wachezaji wake kwa safari ndefu waliyo ipiga kwenye michuano husika. Hajawahi kushinda hata taji moja kubwa.ila mwaka huu alifanikiwa kuingia fainali za UEFA wakicheza na madrid akiwa na kikosi cha vijana walioingiwa na Ule uliva livaa wa kufia uwanjani wakiongozwa na captain wa Henderson na wakiwa na mfungaji machachali Sallah.napo walipoteza wakuwa na kipa wao Karius.

MOHAMED SALLAH EGYPTIAN KING

Nisipo litaja hili jina sitaenda mbingu kwa unafki . Kijana aliefanya mambo ambayo yalimfanya akawa mchezaji bora Africa na kuchukua mfungaji bora wa ulaya akimzidi kane. ALiweza kuibeba Misri mgongoni mwake dakika ya 89 ikicheza na congo na kuweza kuivusha timu yake kwenda kombe la dunia. Alifanya maajabu mengi mpaka ikabidi kMa nchi kuona huyu tusiishie kumuabudu kwenye makaratasi ila tuchukue Viatu alivyochezea kuviweka kwenye makumbusho ya taifa (Adidas X) . Hiki watakiona vizazi na vizazi kua alikuepo mtu aliitwa sallah kwenye soka la Misri.
Kelvin De Brune kiungo bora wa dunia

Takwimu zake ni nzurii sana kuliko Modric , mafanikio yake ni makubwa sana kwa mwaka huu. Huyu mimi ndio ningempa Ballon d’Or kama ningekua natolea kwangu hapa Mbeya basi huyu ningempa. Alichezea Manchester city aliweza kuingoza timu yake kutwaa Epl na yeye binafsi kujishindia Tuzo ya mchezaji Bora wa mwaka kwa Epl. Huyu ndie De brune alieweza kufika nafasi ya Tatu kwenye World Cup ya 2018.

COYS

Totenham hawa ndo timu ilio ongeza kauli ya kutoka Top 4 mpka sasa watu wanaita Top 6. Wamekua nawachezaji wenye vipaji vya hali ya juu sana mpka kupelekea kua timu pekee yenye wachezaji wengi kutoka kwenye kikosi cha timu ya taifa (the three lions). Hii kwangu ni timu ambayo naweza kusema ndio ilikua msingi wa England kufanya vizuri world cup ikiongozwa na striker wao Kane.

Manchester Derby

Huu ndio mwaka ambao ulishuhuudia maasimu hawa wa jiji moja la manchester walikutana wakiwa rekodi zinataka kuandikwa. Hapa zilikutana timu ya kwanza na timu ya pili. Manchester Vity ikiwa inaongoza kwa tofauti ya point 16 ikihitaji pointi 3 kijitwalia ubingwa mbele ya Man United . Huku manchester city ikiwa nyumbani pale Etihad. Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha manchester city ilikua ikiongoza goli mbili kwa moja dhidi ya Manchester United.

Kipindi cha pili kilianzaa na kuona Man United wamerudi kama mbogoo waliochomewa msitu!!.. waliweza kupata Goli mbili nakuwa mbili mbilii na kutetea ushindi wake. Mchezo huu ulishudia pogba akifunga Goli mbili ndani ya dakika 5. Na baada ya muda ndipo Smalling akaihakikishia point tatu United kwa ushindi wa goli la tatu ! Mechii hii ndiyo Mechi Bora iliyo teuliwa Na FA. Hii mechi ilishudia manchester united kugoma kuona Manchester City wanasherekea mbele yao na ndani ya uwanja wao.

.
THE RISE AND FALL OF LEROY SANE. Mjerumani aliebeba tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa Epl. Ila sasa huyu dogo ana historia mbaya na Ujerumani na hii ni baada ya kufanya vizuri sana Epl lakini nchi yake chini ya kocha wao wa taifa Joackim Low kumuacha kwenye kikosi cha ujerumani kilichoenda kucheza world cup huko URusi. Hii ilitikisa mitandao ya kijamii na dunia nzima kuuliza kwanini.. ila kilichowapata kule urusi nadhani hawezi kurudia ule utoto kocha wa ujerumani.
.
.
ENGLAND ITS COMING HOME

Hii ndo timu pekee ilioenda urusi ikiwa na wachezaji wote wa ndani ya ligi yao na ndio timu pekee iliyo chukua nafasi ya 4 kwenye kombe la Dunia . Na kufanya kane kung’ara kwenye mashindano hayo.hii timu ilibebwa sana na wachezaji wa Tot. Hii ndo ligi ya England na huo ndo utamubwake..

Makala kutoka kwa Edger Eddson

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here