Home breaking news EXCLUSIVE: Rais wa Simba hachukui fomu kugombea uongozi

EXCLUSIVE: Rais wa Simba hachukui fomu kugombea uongozi

10861
0

Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah ‘Try Again’ amenithibitishia kwamba hana mpango wa kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya klabu hiyo ikiwa ni pamoja na urais/uenyekiti.

Nikataka kujua kwa nini hataki kugombea urais wakati wadau wengi wa klabu ya Simba wanaamini atagombea urais baada ya kuridhishwa na uongozi wake akiwa kaimu Rais.

Salim ametaja sababu ambazo zimefanya asigombee na kuamua kujiweka pembeni ya mchakato huo.

“Chini ya uongozi wangu nikiwa nakaimu nafasi ya urais nimesimamia mabadiliko ya uendeshaji wa klabu kutoka mfumo wa wanachama kwenda mfumo wa hisa. Endapo nitagombea inaweza kutafsiriwa kuwa nilifanya hivyo nikiwa najitengenezea mazingira ya kuja kuongoza baadaye.”

“Nimefanikisha mchakato huo na sasa Simba ipo kwenye mfumo mpya inatosha, nikigombea ungozi ndani ya Simba kutakuwa na mgongano wa kimasahi.”

“Wakati naingia kwenye uongozi, kwa muda mrefu Simba ilikuwa haijashinda ubingwa wa ligi ya Tanzania. Nashukuru msimu uliopita nimeweza kuiongoza kushinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.”

“Nadhani kwa hayo niliyofanya nikiwa kiongozi ndani ya Simba inatosha, ni wakati wa kuwapisha watu wengine waje kuendelea nilipoishia mimi.”

Leo Jumatatu September 10, 2018 ndio mwisho wa kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Simba kuelekea uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika November 3, 2018.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here