Home Kitaifa Fei Toto kawakata maini wanaoibeza Yanga

Fei Toto kawakata maini wanaoibeza Yanga

12262
0

Na Tima Sikilo

KIUNGO mpya wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, ameweka wazi kwamba kikosi chao kitaendeleza wimbi la ushindi kwenye mchezo wao ujao mbele ya Kagera Sugar kama ambavyo waliwafanyia ndugu zao Mtibwa Sugar.

Fei ambaye amesajiliwa na Yanga kutokea JKU ya Zanzibar, Alhamisi iliyopita alianza majukumu yake ndani ya timu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa ambao Yanga walishinda kwa mabao 2-1.

Akizungumzia mchezo wao ujao, Fei amesema anaamini kikosi chao kinachofundishwa na Mkongo Mwinyi Zahera ‘Papaa’ kitaibuka na ushindi.

“Mashabiki watarajie mengi zaidi ila niwaambie tu kwamba kwenye mpira kuna siku inatokea unacheza vizuri na siku nyingine unacheza chini ya kiwango, huwezi kuwa mkali kila siku. Ninaamini katika mchezo wetu ujao mbele ya Kagera Sugar tutaibuka na ushindi,” amesema Fei Toto

Fei ameongeza kuwa watu wasiichukulie poa Yanga kwani wanauwezo mkubwa wakuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here