Home Kimataifa FIFA yampiga pini kwa miezi 12 raisi aliyewataka Wapalestina kuchoma jezi ya...

FIFA yampiga pini kwa miezi 12 raisi aliyewataka Wapalestina kuchoma jezi ya Messi

9708
0

Chama cha soka ulimwenguni FIFA kimemfungia kwa miezi 12 raisi wa chama cha soka cha Palestina Jibril Rajoub kutojihusisha na masuala yoyote ya soka baada ya kuagiza kuchomwa moto jezi za Lionel Messi.

Fifa kupitia kamati yake ya nidhamu wametoa tamko kuhusu huku ya Rajoub ambapo kifungo hicho kitaendana pamoja na faini kiasi cha £15,826 ambayo raisi huyo atapaswa kulipa kwa kukiuka kanuni za kinidhamu za FIFA.

Mwezi June mwaka huu Rajoub aliandika barua kwa chama cha soka cha Argentina akiwataka wasimchezesha Lionel Messi katika mchezo wa kirafiki kati ya Argentuna na Israel.

Rajoub alitoa onyo kwamba endapo Lionel Messi atakuwepo mjini Jerusalem katika mchezo huo baasi mashabiki wa soka nchini Palestina watafute jezi za Messi popote pale nchini Palestina na wazichome moto.

Rajoub aliishtumu Israel kuhusu mchezo huo na kusema kwamba wanaupeleka kuwa wa kisiasa zaidi na ndio sababu wakaamua mechi hiyo ipigwe mjini Jerusalem jambo ambalo sio sahihi.

Hata hivyo mchezo huo uliahirishwa kutokana na kauli hizo za Rajoub ambapo Argentina walihofia usalama wa wachezaji wao na wakaamua kuachana na mechi hiyo japo FIFA tayari walishafungua kesi dhidi ya Rajoub.

Baada ya kuahirishwa mechi hiyo Rajoub aliibuka tena kuwashukuru Messi na wachezaji wenzake na kusema walichofanga ni sawa na kutoa kadi nyekundu kwa Israel katika soka.

Israel na Palestina wamekuwa katika mgogoro kwa miaka mingi sasa na mgogoro huu unapelekea hata masuala yote ya soka baina ya pande hizi mbili kuonekana kukwama.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here