Home Ligi EPL Florentino Perez amtaja Rafael Nadal kama mrithi wa kiti chake Real Madrid

Florentino Perez amtaja Rafael Nadal kama mrithi wa kiti chake Real Madrid

8236
0

Mcheza tennis maarufu duniani kutoka nchini Hispania Rafael Nadal anafahamika kama moja ya mashabiki wakubwa sana wa klabu ya Real Madrid.

Mwaka 2014 Nadal ndipo aliamua kujiunga rasmi na klabu hiyo na anafahamika katika bodi ya Madrid kama moja ya mashabiki wao wa kutupwa ambao ni maarufu.

Kama hiyo haitoshi mwaka huo huo 2014 Rafael Nadal alihusika katika usajili wa Marco Asensio kutoka Mallorca na inatajwa kwamba ukaribu wao ulimfanya Nadal amshawishi Asensio kwenda Real.

Mwaka 2017 wakati akifanya mahojiano na jarida la As, Nadal alikiri kwamba ilikuwa mapema sana kuongelea uraisi wa klabu ya Real Madrid kwa wakati huo.

“Ni kweli ninaipenda Real Madrid lakini kwa wakati huu sio sahihi kulijadili hili, ila nani anayejua ya mbeleni na ukweli ni kwamba ninatamani kuwa raisi” alisema Nadal.

Sasa hivi majuzi napo raisi wa sasa wa Real Madrid Florentino Perez alikaririwa akisema anadhani mtu anayefaa kuchukia nafasi yake akiondoka kwa sasa ni Rafael Nadal.

Perez akizungumza na jarida la El Confidencial amesema kwamba Nadal atakuwa mtu sahihi sana kwa Real Madrid kutokana na mapenzi yake kwa timu hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here