Home Ligi EPL Fununu: Ndoa ya Mourinho na Man United matatani

Fununu: Ndoa ya Mourinho na Man United matatani

9413
0

Bado kuna fununu zinazidi kuzagaa na kusambaa kwamba klabu ya Manchester united inaweza kuachana na kocha wake wa sasa, Jose Mourinho ambaye amekuwa akiwaalamikia viongozi wa klabu hiyo kwa kutokamilisha usajili wa nyota aliowapendekeza wasajiliwe katika dirisha kubwa la usajili ambalo kwa nchini Uingereza lilifungwa tarehe 9-Agosti.

Lakini huu ni kama mzimu unaoendelea kumfatilia kocha huyo kutokana na rekodi yake mbovu ya kutimuliwa na klabu anazozifundisha kila baada ya misimu mitatu au chini ya hapo.

Katika maisha yake yote ya ukocha amekuwa hamalizi msimu wa tatu na kusalia na klabu na huenda hili likaenda kutokea msimu huu akiwa na Mashetani Wekundu.

Alijiunga na Manchester united mwaka 2015 mara baada ya kutimuliwa na Chelsea ambapo huko alidumu kwa misimu miwili na nusu, na moja ya sababu zinazotajwa kumfanya kutimuliwa Chelsea ni kuwa na mahusiano mabaya kati yake na nyota wa Chelsea wakiwemo Eden Hazard na Diego Costa.

Na huenda hilo nalo likajirudia kwasasa ambapo inahisiwa kwamba mahusiano yake na kiungo raia wa Ufaransa klabuni hapo, Paul Pogba hayapo vizuri.

Unadhani kipi Mourinho anakiwaza kwasasa? hii ni filamu kali ambayo dunia inasubiri kuona mwisho wake utakuwaje?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here