Home Kimataifa Gattuso vs Anceloti, mwalimu na mwanafunzi wake kuoneshana ubabe. Ni Napoli vs...

Gattuso vs Anceloti, mwalimu na mwanafunzi wake kuoneshana ubabe. Ni Napoli vs Ac Milan

9551
0

Leo ni kati ya wikiendi tamu sana kwa sisi watumiaji wa DSTV kwani ni bandika bandua, Serie A leo moto hauzimi. Wakati Cr7 akiwakabili Lazio, kuna hii mechi kati ya Ac Milan vs Napoli.

Kama unakumbuka Gennaro Gattuso alikuwepo katika kikosi cha Ac Milan ambacho kilinolewa na Carlo Ancelotti 2001-2009 ambacho kilibeba jumla ya makombe 9 barani Ulaya.

Kwa wakati huo Gattuso alikuwa akiichezea Ac Milan. Lakini miaka kadhaa baadaye Gattuso anakutana na Anceloti huku wote wawili wakiwa makocha, Gattuso Ac Milan, Anceloti Napoli.

Achilia mbali kwa Ancelotti kushinda makombe makubwa Ulaya mwaka 2003 na 2007 kama kocha wa Milan lakini amewahi kubeba European Cup mara mbili kama mchezaji wa Milan(1989 na 1990), lakini yote hayo atasahau hii leo na kujaribu kuichapa Milan.

Gattuso ana kazi kubwa kuepuka kipigo kutoka kwa Napoli kwani Ac Milan katika mechi zao 7 zilizopita hawakupata ushindi hata mechi moja mbele ya Napoli, wakipigwa 5 na suluhu 2.

Hofu kubwa kwa Milan ni kwamba Fabio Borini hana uhakika wa kucheza hii leo huku Hakan Calhanoglu akiwa anatumikia adhabu ya kadi na hii inaleta hofu nani atakayecheza upande wa kulia katika 4-3-3 ya Gattuso.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here