Home Kimataifa Georgino Wijnaldum ni shujaa asiyeimbwa Anfield

Georgino Wijnaldum ni shujaa asiyeimbwa Anfield

5075
0

Geogino Wijnaldum ni kiungo wa Liverpool asiyeimbwa sana baada ya mechi kama walivyo akina Keita na wengineo.
Moja ya sifa kubwa ya Wijnaldum, ni namna anavyojitoa kwaajili ya timu. Anakupa asilimia 100 ya kila kitu chake. Mpira ni kipaji na kujituma. Vitu vyote hivyo ukiwa navyo huwezi kuanguka.

Kocha Jurgen Klopp anaelewa umuhimu wa Georgino ndomaana anampanga hata kwenye zile mechi muhimu. Pengine ni mchezaji wa mechi kubwa. Sio rahisi kuiba mpira kwa Geogino Wijnaldum. Anakokota mpira akiwa na nguvu, kasi, na kuweza kumudu kasi ya mchezo.

Miguu yote miwili ina nguvu. Mashabiki wanaoelewa kazi yake wanakwambia ni bahati kuwa na mtu anayeweza kujitoa ili timu ishinde. Hawajiulizi maswali mengi kwanini hafungi magoli wakati ana uwezo mkubwa wa kucheza hata namba kumi.

Haumii mara kwa mara, anampa njia mbadala Klopp. Ukiwa na mchezaji asiyeumia mara kwa mara inabidi ujivunie kuwa naye maana anakupa matumaini muda wowote hata kama mambo ni magumu.

Wijnuldum huwezi kuona ametawala dimba la katikati, huwezi kuona akiufanya mpira anavyotaka, lakini kitu muhimu ni kuipambania timu yake. Hachoki. Akiwa na James Milner, kazi yao inaonekana. Kuna wakati kocha hategemei kipaji kutoka kwa mchezaji. Anataka ujitume. Bahati nzuri Klopp ana uwezo mkubwa wa kuboresha viwango vya wachezaji. Mchezaji anaweza kuwa wa kawaida sana lakin akiwa chini ya Klopp lazima aimarike inavyotakiwa.

Ujumbe kutoka kwa Admila Patrick


PATA KIFURUSHI

Liverpool Vs City: Usajili

City walitoa 45 milioni kwa Mendy
LFC walitoa 8 milioni kwa Robertson

City walitoa 36 milioni kwa Gundogan
LFC walitoa 20 milioni kwa Wijnaldum

City walitoa 55 milioni kwa Mahrez
LFC walitoa 13 milioni kwa Shaqiri

Kimahesabu hapo City wametumia zaidi ya 95 milioni kupata wachezahi ambao ninsawa tu na wale wa Liverpool.


Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here