Home Kimataifa Giroud avunja rekodi ya Zidane, Ufaransa yaifunga Uholanzi kwa tabu sana

Giroud avunja rekodi ya Zidane, Ufaransa yaifunga Uholanzi kwa tabu sana

11670
0

Mchezo wa kundi la kwanza  kwa upande wa ligi daraja la A la michuano ya Uefa National Leguae  imekamilika kwa Ufaransa kuibuka kidedea kwa kuwaafunga Uholanzi mabao mawili kwa moja.

Mabao ya Kylian Mbappe na Oliver Giroud yalizamisha meli ya kidachi. Giroud amefunga baada ya ukame wa takribani dakika 801 tokea afunge bao lake la mwisho kwa timu yake ya taifa ya Ufaransa. Katika mchezo huo ilimchukua idadi ya mashuti matatu kabla ya Giroud kujipatia bao lake.

Bao la Uholanzi lilifungwa na Ryan Babel mchezaji wa zamani wa Liverpool. Babel alipiga mashuti mawili pekee.

Kipa wa Uholanzi Cillessen alifanya kazi ya ziada kuokoa hatari 6 katika lango lake, huki Areola akiokoa shuti moja pekee lililokuwa na hatari langoni mwake.

Ufaransa walimiliki mpira kwa asilimia 53.7 huku wageni wakamiliki kwa asilimia 46.3. Wafaransa walipiga mashuti 15 huku upande wa pili wakafanikiwa kupiga mashuti 7. Wafaransa walifanikiwa kupiga pasi 598 dhidi ya pasi 50u za wapinzani wao. Upande wa kushoto wa Ufaransa ulionekana kuwa na nguvu zaidi katika mchezo huu.

Kwa upande wa Ufaransa Giroid ndiye mchezaji aloyeongoza kwa kupoteza mpira mara nyingi zaidi mara 6, na kwa Upande wa Uholanzi ni Depay mara 5.

Varane aliongoza kwa kubloku mpira mara nyingi zaidi kwa upande wa Ufaransa mara 3, vivyo hivyo kwa ligt alibloku mara 3 kwa upande wa Uholanzi.

Babel aliotea mara 1, huku Mbappe akiotea mara 2. Wafaransa waliokoa mpira mara 26, Varane akiongoza kwa kuokoa mara nyingi zaidi mara 9, huku Waholanzi wakiokoa mashambulizi ya hatari mara 23, Blind na ligt wakiongoza na wote waliokoa mara 6.

Msimamo wa kundi hilo.

P W D L Pts
France 2 1 1 0 4
Germany 1 0 1 0 1
Netherlands 1 0 0 1 0

Mchezo ulikuwa wa kasi sana lakini kilichowasiadia Ufaransa ni uzoefu mkubwa waliokuwa nao ukilinganisha na wapinzani wao. Mbappe sasa yupo kwenye kiwango bora baada ya kufunga mabao 9 kwenye michezo 12 iliyopita kwa taifa na klabu yake. Oliver Giroud amevunja rekodi ya Zinedine Zidane ya kufunga mabao mengi kwa Ufaransa (32) huku zidane akiwa amefunga mabao (31).

Giroud anashikilia nafasi ya 4 kwa kufunga mabao mengi timu ya taifa.

Matokeo na mechi zijazo la kundi hili.

Germany 0:0 France 06.09.18
France 2:1 Netherlands 09.09.18
Netherlands -:- Germany 13.10.18 20:45
France -:- Germany 16.10.18 20:45
Netherlands -:- France 16.11.18 20:45
Germany -:- Netherlands 19.11.18 20:45

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here