Golikipa Metacha Mnata wa Mbao FC ya Mwanza amechaguliwa kuwa golikipa bora wa mashindano ya SportPesa Cup 2019, baada ya kuonesha uwezo wa juu mashindano hayo.
Katika dakika 270 (mechi tatu) alizocheza, ameruhusu goli 1 (Mbao FC 1-1 Gor Mahia) ukiachana na mikwaju ya penati kwa ajili ya kuamua mshindi ili kufuzu hatua inayofuata.
Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano hayo licha ya timu yake kufungwa na Simba kwa penati 5-3, Metacha aliibuka mchezaji bora ‘Man of the Match’ wa mchezo huo.
Hongera sana kijana kwa kutumia vizuri fursa👏 Safari mpya huenda ikaanzia hapa!!
Full video tayari ipo #YouTube ingia #DaudaTV umfahamu Metacha. mwanzo mwisho.